Mkurugenzi mtendaji wa hospitali za Apollo Dr.
Hariprasad akiwahutubia wadau wa afya hivi karibuni. Hospitali ya Apollo
inaamini katika kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Dar es Salaam, Septemba,
2014. Ukosefu wa
huduma za afya za uhakika na za kisasa zinadaiwa kuwa sababu kubwa ya watanzania wengi kufuata huduma hizo nchi za nje.
Hospitali ya Apollo ilikuwa moja ya hospitali
za mwanzo kabisa katika bara la Asia, na duniani kwa ujumla kuleta huduma zote
za kiafya chini ya paa moja. Na kwa wakati huu, mpango huo kabambe umeifanya
hospitali hiyo kufanikiwa katika Nyanja zote za matibabu.
Dr.
Prathap C Reddy, muasisi wa huduma za kiafya za kisasa nchini india, alianzisha
hospitali ya aina yake nchini humo mwaka 1983. Ikitoa huduma zote za kiafya,
hospitali ya Apollo ina zaidi ya vitanda 8000 katika jumla ya hospitali zake
zipatazo 50, na idadi ya maduka ya dawa baridi yapatayo 50, vituo vya afya vya
uchunguzi wa kina, vituo vya bima za afya pamoja na uchunguzi wa kina wa seli
mbalimbali kwa ajili ya utafiti. Hospitali ya Apollo ni hospitali bingwa duniani
kwa upandikizi wa viungo mbalimbali vya binadamu duniani.
Nchini
Tanzania, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kama saratani,kisukari, na magonjwa
yanahusiana na moyo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi. Magonjwa haya yamesababisha
kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na pia yanagharimu fedha nyingi ambazo
zingeweza kutumika kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi.
Hivi
sasa, uwezo wa Tanzania kutibu magonjwa ya moyo, upasuaji wa moyo, saratani, na
matatizo ya figo ni mdogo, na maelfu ya watanzania hufuata huduma hizi nje ya
nchi kwa bei nafuu, hususani nchini India.
Ugonjwa wa moyo ni wa pili kwa kusababisha vifo vingi nchini Tanzania
baada ya malaria, ukichangia vifo 287 kwa siku, au 104,755 kwa mwaka, kwa
takwimu za taasisi ya moyo Tanzania. ‘Tanzania kwa sasa haina kituo maalum cha kutoa matibabu ya jumla ya moyo.
Asilimia 20 ya vifo vyote hutokana na ukosefu wa utaalamu, vifaa na umaskini,
na wale wenye uwezo inawabidi kusafiri nje ya nchi,’
Inaongeza taasisi
hiyo katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, safari ya hospitali ya
Apollo imetengeneza historia ya kupendeza katika hali nzima ya utoaji wa huduma
za kisasa za afya nchini India. Taasisi hiyo imeendelea kung’ara kati ya watoa
huduma binafsi. Hospitali hii ilikuwa moja ya waanzilishi wa tuzo za juu za
utoaji wa huduma ya kisasa duniani.
Hospitali ya Apollo ni moja ya hospitali zinazojulikana vyema miongoni
mwa wa-Tanzania, kwani viongozi wengi maarufu, wafanyabiashara na mamia ya
wagonjwa wenye uhitaji wa upasuaji wamekuwa wakisafiri na kupata matibabu kutoka
hospitali hizi maarufu.
Hivi karibuni hospitali ya Apollo ilifanya upasuaji wa kuwatenganisaha
mapacha kutoka Tanzania kwa mafanikio makubwa.
Nchi za India na Tanzania zimekua na ushirikiano mkubwa kihistoria,
kiutamaduni, kisiasa na kibiashara, na uwepo wa hospitali hizo nchini Tanzania utaendelea
kudumisha uhusiano mwema kati ya nchi hizi mbili.
Zaidi kuhusu
hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo
ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa
kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa
karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika
elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".
Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo
imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni
kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika
sekta ya afya nchini india.
Katika safari yake, imeweza
kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.
Inatoa huduma maalum 52 na
vitanda vya upasuaji 710
Imefanya upasuaji wa moyo
wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.
Imefanya upasuaji wa wa
viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo,
uti wa mgongo na zaidi.
Taasisi ya Apollo ni moja
ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama
Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.
No comments:
Post a Comment