Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, (UNDP), limetoa fedha kiasi cha
shilingi milioni 39, kwa Shirika lisilo la kiserikali la TEACA, kwa
lengo la kuendeleza mradi wa mazingira, katika mtandao wa
vijiji 37 ili kuweza kurejesha uoto wa asili ambao umeanza kupotea
katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Makamu Mwenyekiti wa shirika hilo, Adoncome Mcharo,
ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya shirika hilo,
kwenye mkutano mkuu wa 18 wa shirika hilo.
Amesema taasisi hiyo imekuwa ikiendelea na shughuli zake
za kupambana na kuhifadhi wa mazingira na kuyaendeleza ikiwa ni
pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mazingira bora kwa
viumbe hai.
Mcharo amesema Uharibifu wa
mazingira ni kosa ambalo limekuwa likifanywa na binadamu, na kutoa
wito kwa, wananchi kujitahidi kuendelea kuyaunza
mazingira hayo ili yasiendelee kuharibiwa.
Amelipongeza shirika la UNDP kwa kuona umuhimu wa kuweza
kuwasaidi fedha hizo kutokana na maeneo mengi ya wilaya ya Moshi
kuharibiwa na wananchi wachache kwa manufaa yao binafsi.
Amesema changamato kubwa iliyopo
kwa sasa ni kuendelea kuwaelimisha wananchi umuhimu wa utunzaji
bora wa mazingira na dhamana ya kuilinda misitu hiyo.
Aidha ameongeza kuwa TEACA,
imeanza kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, ambapo wameanza kwenye
shuule za msingi na sekondari zilizopo katika wilaya ya Moshi.
No comments:
Post a Comment