Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, September 12, 2014

UMWAGAJI WA DAMU KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WANUKIA KILIMANJARO NA ARUSHA

SERIKALI imetakiwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 kati ya wafugaji na wakulima wa wilaya za Siha mkoani Kilimanjaro na Arumeru mkoani Arusha kutokana na kuwepo kwa hatari kubwa ya umwagikaji wa damu.

Agizo hilo lilitolewa jana wilayani Siha mkoani Kilimanjaro na Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Kilimanjaro, Deogratias Rutta wakati akikagua miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Siha. Rutta alisema mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 kati ya wafugaji wa kijiji cha Lekirumuni wilayani Siha na wakulima wa kijiji cha Olkugwado wilayani Arumeru sasa umeingia katika sura mbaya zaidi na kwamba iwapo serikali kama haita chukua hatua madhubuti za kutatua mgogoro huo ni dhahiri kuwa damu zitamwagika.

Alisema nchi ya Tanzania kwa sasa imekuwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo imegharimu maisha ya watu kutokana na mapigano ya mara kwa mara hususani ile ya wafugaji na wakulima na kwamaba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kumaliza migogoro hiyo. Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Lekrumuni Moses Mollel, alisema mgogoro huo ulianza tangu mwaka 1996 ambapo wakulima wa kijiji cha Olkugwado kutoka wilayani Arumeru walivamia eneo lililotengwa kwaajili ya wafugaji na kuanza kulima mazao mbalimbali ikiwemo nyanya.

Mollel alisema mgogoro huo unasabaisha na kutokutambuliwa kwa mipaka kati ya wilaya ya Siha na Arumeru na kwamba mgogoro huo umekwisha leta madhara makubwa ikiwemo umwagaji wa damu na kufyekwa kwa mazao ya wakulima. Aidha alisema licha ya serikali kuingilia kati na kuibainisha mipaka hiyo lakini bado tatizo hilo limeendelea kila mwaka na kwamba limekuwa likiwakosesha amani wafugaji katika maeneo yao na kuitaka serikali kumaliza tatizo hilo haraka kabla ya vita vya wakulima na wafugaji kuanza.

Nae Diwani wa kata ya Karansi Dankani Urassa, alisema ni vyema sasa serikali kupitia wizara ya ardhi kutuma wataalamu kuja na kufanya uhakiki wa mipaka hiyo na kuwaonesha mipaka hiyo wakulima kutoka katika wilaya Arumeru ili kuacha tabia ya kuvamia katika maeneo ya wafugaji na kusababisha migogoro isiyo kuwa na tija. Dankani alisema mgogoro huo umekwisha kutatuliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuushirikisha uongozi wa wilaya na mkoa lakini jitihada hizo zimegonga mwamba kutokana na kwamba mpaka sasa hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Akizungumzia mgogoro huo Mkuu wa wilaya ya Siha, Dkt. Charles Mlingwa, alisema serikali ya wilaya tayari imekwisha shughulikia tatizo hilo toka mwaka jana na mpaka sasa hawajapata taarifa za kuwepo kwa malumbano hayo na kwamba suala la mipaka haliwahusu lipo katika wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI.

No comments:

Post a Comment