Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, September 12, 2014

WAUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI KILIMANJARO WAANDAMANA

KILIMANJARO baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi iliyoko mjini Moshi, walikusanyika katika ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Kilimanjaro, wakidai kurudishiwa fedha zao za bima ya afya walizokatwa katika mishahara yao.
Wakiongea kwa sharti la kutokutajwa kwenye vyombo vya habari baadhi ya wafanyakazi hao walisema walikatwa fedha zao kwenye malipo ya mishahara ya miezi mitatu.
Walisema wafanyakazi wa halmashauri zingine walishalipwa fedha zao na kwamba wao bado hawajapata haki zao na wanapofuatilia swala hilo baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wamekuwa wakiwapa majibu yasiyo ya kuridhisha ikiwemo kuwakejeli.
Akiongea na wanahabari kuhusiana na swala hilo, meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kilimanjaro, Fidelis Shauritanga, alikiri kuwepo kwa makosa hayo na kusema kuwa tayari ofisi hiyo ilisharudisha fedha hizo ofisi ya katibu tawala mkoani wa mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema katika ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, wanachama 178, walibainika kukatwa kimakosa na Shilingi Milioni 7,539,612 zililipwa katika ofisi ya Ras toka mwanzoni mwa mwezi julai mwaka huu 2014.
Alisema ya kuwa kwa hali hiyo ofisi ya bima ya afya ilishatimiza wajibu wake na kwamba haipaswi kunyooshewa kidole cha lawama kutoka na mtu mwingine kushindwa kuwajibika.
Meneja huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka waajiri ambao hawajawasilisha fedha hizo kwa watumishi waliokatwa, kuwasilisha mara moja, ili kuwaondolea watumishi hao, usumbufu ambao wamekuwa wakiupata.
Akiongelea swala hilo katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Faisal Issa, alikiri kuwepo kwa kasoro hiyo na kwamba tayari limeshaanza kushughulikiwa.

No comments:

Post a Comment