Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 9, 2014

WANAFUNZI WAWILI WA SHULE YA SECONDARY WANASHILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

ROMBO wanafunzi wawili wa shule wa ya sekondari ya Makiidi iliyopo wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wanashikiliwa na Jeshi polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi wa shule ya msingi Maureni iliyopo Mkuu wilayani Rombo. Mwenyekiti wa kijiji cha Makiidi, Rogath Namfua alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba alisema lilitokea Septemba 5 mwaka 2014 majira ya saa sita mchana na kwamba wanafunzi hao walimvamia mwanafuzi wa shule ya Msingi Maureni ambaye anasoma darasa la pili na kumbaka. Namfua alisema wanafunzi hao walimvamia mwanafuzi huyo wa darasa la pili wakati akirudi kutoka shuleni na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama. “Walimvamia mtoto huyo na kumpeleka shambani na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama mwanafunzi huyo wa darasa la pili na kumuumiza vibaya sehamu za siri” alisema mwenyekiti huyo. Alisema mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Huruma na kupatiwa matibabu na kwamba kwa sasa yupo nyumbani anaendelea na dawa. Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuthibitika kuwa mwanafunzi huyo aliingiliwa na wanafunzi hao walikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi cha wilaya ya Rombo. kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanafunzi hoa wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment