MOSHI mtu mmoja kati ya watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
amemiminiwa risasi kadhaa mwilini na kufariki dunia papo hapo, kwa kile
kilichodaiwa kuwa alijibizana kwa kurushiana risasi za moto na askari wa
jeshi la polisi wa kituo cha polisi Himo, katika eneo la njia panda
Himo, mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boas, alisema aliyeuawa
hajatambulika kwa jina lakini inasadikiwa kuwa ni raia wa nchi jirani,
ambapo kamanda huyo hakuwa tayari kuitaja nchi hiyo kwa sababu za
kiupelelezi.
Amewataja wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni, Edimund Ludoviki (36),
mkazi wa Rombo, ambaye amekuwa akihusishwa na matukio mbalimbali ya
unyang’anyi kwa kutumia silaha za moto, katika mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro na Endrick Ngomuo (30), ambaye ni mkazi wa makuyuni himo.
Marehemu huyo baada ya kuuawa alipekuliwa na kukutwa na bastora aina ya
Cheinis ikiwa na risasi 12, pamoja na kofia za kuziba uso (mask).
Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, kamanda Boas amesema watu hao
walikutwa wakiwa bar inayoitwa Gozar inayomilikiwa na Mery Mauki, baada
ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema za kuwepo kwa majambazi hao
ambayo walikuwa wakijiandaa kupora.
No comments:
Post a Comment