Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 6, 2014

Mama mzazi afanyia mwanae ukatili wa kutisha kwa kumkata mtoto nyama mapajani na kuichoma jikoni


KILIMANJARO vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani Kilimanjaro vimezidi kushika kasi ambapo mtoto mwenye umri wa miaka (8), jina limehifadhiwa amefanyiwa kitendo cha ukatili na Mama yake mzazi ambaye  anadaiwa kumkata mwanawe nyama katika eneo la paja la mguu na kuiweka kwenye moto.

Mwanamke huyo, Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya kitendo hicho dhidi ya mtoto wake wa kiume wa kumzaa, baada ya kurejea nyumbani kutoka kwenye shughuli zake akidhaniwa alikuwa analewa.

Akizungumza katika Hospitali ya Kibosho alikolazwa hivi karibuni, mtoto huyo anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Sungu, mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilolifanya hadi mama yake akachukua uamuzi wa kumkata.
 
Mtoto huyo alisema kwamba mama yake alifika nyumbani na kumkuta, ndipo akaenda jikoni akachukua kisu na kumkata nyama kwenye paja kisha akaenda kuichoma na wakati ikifuka moshi na kutoa harufu akaichukua na kuanza kumwekea puani.

Inadaiwa kuwa Baba wa mtoto huyo alishafariki dunia na inadaiwa kwamba mama huyo amekuwa na tabia ya kulewa pombe na pia hufanya kazi ya kutengeneza pombe ya  kienyeji ya mbege huko Maua.

Katibu wa taasisi ya Kuwatembelea Wagonjwa Majumbani (WAKUWANYU) Tarafa ya Kibosho, Paul Lazaro alisema kuwa mtoto huyo ni mmoja wa wale wanaopatiwa huduma yao kwa sababu anaishi katika mazingira magumu kana kwamba ametelekezwa.

WAKUWANYU,  inafanya kazi chini ya taasisi ya Jimbo katoliki Moshi ya Rainbow, ambapo huwaangalia wagonjwa wa aina mbalimbali, wakiwamo wenye upungufu wa kinga mwilini, wasiojiweza na wenye magonjwa mengine.

Lazaro ambaye alifika hospitalini kumtembelea mtoto huyo pia, alieleza kusikitishwa kwake na kitendo hicho na akina mama kadhaa walikuwa wakijiuliza kulikoni hadi mwenzao amfanyie ukatili mkubwa kiasi hicho mwanawe wa kumzaa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alikiri tuhuma za mama huyo kumnyanyasa mwanawe na kumpiga Bernadeta na kwamba uchunguzi umefanyika na jalada kupelekwa kwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ambaye amebaini kuna kesi ya msingi.

No comments:

Post a Comment