Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 28, 2014

Tatizo la fedha bandia lazidi kuota mizizi katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro

KILIMANJARO tatizo la kugushi fedha na kuziingiza kwenye mzunguko sambamba na fedha halali, limetajwa kuendelea kuota mizizi katika baadhi ya maeneo kanda ya kaskazini, jambo ambalo limekuwa likisababisha madhara makubwa ikiwemo kupunguza thamani ya fedha halisi.

Katika Kanda ya Kaskazini, Mkoa wa Arusha unatajwa kuongoza kwa kuwana matukio mengi ya fedha bandia, ukifuatiwa na mkoa wa Manyara na Kilimanjaro ikishika nafasi ya Tatu.


Hayo yalibainishwa jana na Meneja kitengo cha uchumi katika benki kuu ya Tanzania Tawi la Arusha Wilfred Mbowe, wakati akizungumza kwenye semina na wajumbe wa  kamati ya ushauri ya mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa huo mjini Moshi, kwa lengo la
kuwasilisha maendeleo ya uchumi katika mkoa huo.


Mbowe alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 mkoa wa Arusha yaliripotiwa matukio ya fedha bandia kwa asilimia 15.1, ambapo matukio yalikuwa matatu na noti bandia zilikuwa 48 za shilingi 10,000 na noti 38 za Sh. 5,000,huku mwaka 2013/2014 yakiongezeka hadi kufikia asilimia 54, ambapo Noti zilizokamatwa zilikuwa 102 za Sh. 10,000 na
Noti 23 za Sh. 5,000.


Alisema katika mkoa wa Manyara mwaka 2012/2013, uliongoza kwa kuwa na asilimia 76 lakini mwaka 2013/2014, ilipungua hadi kufikia asilimia 36, huku katika mkoa wa Kilimanjaro yakipungua kutoka asilimia 8.8 mwaka 2012/2013 hadi kufikia asilimia 8.3 mwaka 2013/2014.


Aidha alisema ili kuweza kupambana na uhalifu huo Benki kuu imeongeza ubora kwa kuweka alama maalumu za usalama,kutumia utaalamu mpya pamoja na kuziimarisha.


Mbowe alitumia pia nafasi hiyo kuwataka wananchi,kuwa waangalifu na kuzichunguza fedha za noti wanazopokea hasa wakati wa giza,na kutambua kuwa ni kosa kisheria kughushi noti ya fedha, na atakayebanika atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichozidi miaka mitano.


Kwa upande wake Edwin Mtui ambaye ni Afisa wa Benki kuu tawi la Arusha, alisema kumekuwepo  na utunzaji mbaya wa fedha za noti, ambao hupelekea kuchakaa na kupunguza muda wa kukaa kwenye mzunguko,hali ambayo hulisababishia taifa kutumia gharama kubwa ya kuchapisha fedha mara kwa mara.


Alisema uchapishaji wa Noti mara kwa mara,hupunguza gawio la Benki kuu kwa Serikali na hivyo kupunguza uwezo wa serikali kugharamia shughuli zake, hivyo wanancho wote wana wajubu wa kuhakikisha wanatunza vizuri fedha, ili kuweza kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake kwa
malengo yaliyokusudiwa.


Hata  hivyo alizitaka taasisi za fedha zilizoko mkoani Kilimanjaro,kutoa elimu kwa wafanyakazi wake, hasa wale ambao wanajihusisha na kupokea au kulipa fedha, ili kuweza kutambua fedha bandia kabla hazijaingia kwenye mfumo wa Benki ikiwa ni pamoja na kutumia mashine za kuhesabia fedha, zenye uwezo wa kutambua fedha
bandia” alisema.

No comments:

Post a Comment