Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 5, 2015

Majambazi wavamia na kupora bastola aina ya beretta na vitu vingine vya thamani

KILIMANJARO jeshi  polisi mkoani Kilimanjaro linawasaka watu 10 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia nyumbani kwa mtu mmoja na kupora mali mbalimbali ikiwemo bastola aina ya Beretta yenye nambari  E9B3K2Y.



Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Geofrey Kamwela alisema tukio hilo lilitokea Januari tano mwaka huu majira ya 10:00 alfajiri katika kata ya Ngangamfumuni katika Manispaa ya Moshi mkoani hapa.



Akielezea mazingira ya tukio hilo kamanda Kamwela alisema kundi la majambazi hao walivamia nyumbani kwa Gervas Mulokozi (64) wakiwa na silaha mbalimbali za jadi ikiwemo Mapanga, Marungu na fimbo na kisha kumshambulia  na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.



Alisema watu wengine walio jeruhiwa katika tukio hilo ni  pamoja na mkewe Advenika Mulokozi  (58)  muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi  na kujeruhiwa kwa kupiga marungu kichwani na mkononi pamoja na mtoto wake Janath Mulokozi (25).



Alisema mara baada ya uwajeruhi kwa watu hao walifanikiwa kupora bastola hiyo, Deki moja ya DVD, Simu sita za aina tofauti tofauti zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane, funguo za magari pamoja na vitu vingine mbalimbali  ambavyo thamani yake bado haijajulikana.




Aidha alisema majeruhi wote wamelazwa katika hosptali ya Mawenzi kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment