Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, January 5, 2015

Wanafunzi watimuliwa na kuishia kulala stendi ya mabasi kwa kushindwa kulipa ada kwa wakati

Wanafunzi  zaidi 100  wanaosoma katika chuo cha uuguzi cha huruma"Huruma nursing college" wamelala katika stendi ya madasi ya rombo mkuu baada ya kufukuzwa usiku na kuzuiliwa kuingia chuoni hapo na uongozi wa chuo hicho  kwa kushindwa kukamilisha ada.

Wanafunzi hao  wamejikuta katika wakati mgumu usiku wa januari  4 mwaka huu, baada ya kutimuliwa  na kuzuiwa kuingia katika eneo la chuo kwa  kile kinachoelezwa kuwa walishindwa kukamilisha ada zao na michango mingine ya chuo.

Wanafunzi hao  wanasema wamelazimika kulala  katika stendi hiyo ya mabasi mkuu wakisubiri kutumiwa fedha na ndugu zao kwani wengi wao hawakua na fedha za kulipia sehemu ya kulala. 

Mmoja wa wakazi wa rombo mkuu, Ester Tarimo, alisema "wanafunzi wa chuo hicho walikuwa wakiranda randa ovyo usiku mitaani wakiwa na mabegi yao pamoja na vifaa vya shule kutokana na kufukuzwa usikuu huo na kukosa sehemu ya kulala."

Tarimo alisema uongozi wa chuo hicho haukufanya vizuri kuwafukuza wanafunzi hao usiku  na kwamba wangetumia busara wawarudishe asubuhi kwa kuwa kulikuwa hamna madhara yoyote ya kuwaacha chuoni hapo.

Mmoja wa wanafunzi hao John Shija ambaye mzaliwa wa Mwanza, alisema  tarehe tatu ndipo aliporipoti chuoni hapo akitokea nyumbani na kutimuliwa usiku huo kwa kuwa hakuwa amemaliza kulipa ada.

Alisema aliwaomba uongozi huo kuwavumilia kwa kuwa wazazi wao wangetuma fedha hizo lakini hawakuwasikiliza na kuwatoa nje na kuamuru mlinzi kutoruhusu mwanafunzi kuingia chuoni hapo usiku huo.

“sisi tulifika hapa saa kumi na mbili jioni ya tarehe 3 tukaambiwa hakuna ruhusa ya kuingia chuoni tukaambiwa tusubiri ilipofika saa mbili usiku tukafukuzwa tukawaomba kwamba tumeshawapigia wazazi wetu simu wanatuma hela lakini hawakutaka kutusikiliza kabisa” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Aidha walisema  kuwa kwa sasa wanaishi kwa shida kwani wengi wao hawana uwezo wa kulipia nyumba ya kulala na pia kurudi kwao ni mbali “mimi natokea mkoa wa mwanza tangu tarehe 3 nipo hapa siwezi kurudi kwetu ni mbali na hela ya kulipia nyumba ya wageni sina sijui nitafanyaje naomba tusaidiwe jamani”alisema Shija

Walisema utaratibu huo wa kulipa ada kwanza ni mpya na kwamba wazazi  hawakushirikishwa kuhusu utaratibu wa ulipaji wa michango ya shule ili kuepusha usumbufu usio wa lazima kwani wazazi ndio wangetakiwa  kulipa na sio kuadhibu wanafunzi.

Akizungumzia suala hilo Kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Hicho sista Evarista Lasway ambaye imeelezwa kuwa ni Mgonjwa mwakilishi wa Mkuu huyo wa Chuo Sista Florence, amekiri kufukuzwa kwa wanafunzi hao ambapo alisema kuwa ni utaratibu ambao walijiwekea na wanafunzi hao kabla ya
kufunga chuo na hivyo sio suala la kushtukiza.

Sista Florence alisema  kuwa wazazi wa wanafunzi hao walipewa  walishirikishwa kuhusiana na maamuzi mapya ya bodi ya chuo hicho waliwapigia simu wazazi na kuwaeleza kuwa  wawasilishe kwa wakati michango ya chuo  na walioshindwa kufanya hivyo ndio walioofukuzwa.

No comments:

Post a Comment