Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, April 25, 2015

Hospital ya KCMC yashindwa kutumia teknolojia ya kisasa kuhudumia wagonjwa
KILIMANJARO wananchi wanaoenda kupata huduma ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mkoani Kilimanjaro, wamelalamikia utaratibu wa kupata huduma katika hospitali hiyo kutokana na kubadilisha mfumo wa malipo kufanywa kwa kadi ya Benki yaani Tembo kadi.

Wameendelea kudai kuwa, teknolojia hiyo imekuwa ikisababisha kero kubwa  na adha kwa wananchi kutokana na muda mwingi huduma hiyo kukosekana kutokana na tatizo la mtandao na kuwasababishia wananchi kukaa katika foleni kwa muda mrefu bila kupata huduma ya kumuona daktari.

Mmoja wa wananchi Aisha Ramadhan amesema kuwa, Seriakali hususani wizara ya afya inapaswa kuangalia swala hili kwa jicho pevu, kwani wananchi wamekuwa wakienda hospitalini hapo wakiwa na wagonjwa wenye hali mbaya, lakini wamekuwa wakinyimwa kumwona daktari au kupatiwa huduma yoyote mpaka watakapokata kadi ya Benki.

Ameendelea kudai kuwa, unapofika katika dirisha la kukatia kadi hiyo unakuta msongamano mkubwa kutokana na mtandao kutokufanya kazi, ambapo wanalazimika kusubiri huduma, huku mgonjwa akiendelea kupata maumivu.

Mwananchi mwingine, Juma Issa amesema kuwa, wananchi wengi wanaokuja kupata huduma ya Afya katika hospitali hiyo, wamekuwa wakiondoka bila kupatiwa huduma na kwenda hospitali binafsi kutokana na kukaa katika foleni ya kukata kadi ya Benki kwa muda mrefu bila kupatiwa huduma.

Issa amesema kuwa, Uongozi wa Hospitali hiyo umeiga taaluma za ulaya, bila kuangalia kuwa je watanzania tutaweza kuzitumia na pia vifaa vya kutolea  huduma hiyo tunavyo, hali inayosababisha wagonjwa wengi kuzidi kuumia kwa kutopatiwa huduma yoyote hata dawa ya kutuliza maumivu, huku wengine wakifariki bila hata kuonana na daktari.

Mwanahabari wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiwa katika dirisha la kuchukulia kadi hizo za Benki, wakiwa katika Foleni, huku huduma hiyo ikiwa imesimama kutokana na mtandao kutokufanya kazi, na wagonjwa wakiwa wamelazwa na wengine wakiwa wamekaa katika vitanda na viti vya kupokelea wagonjwa walio maututi, na wakiwa hawajapatiwa huduma yoyote wala kumwona daktari.

No comments:

Post a Comment