Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, April 21, 2015

Watu wawili wauwawa katika tukio la ujambazi eneo la Soweto mjini Moshi

Mashuhuda wa tukio hilo la mauaji wakishangaa mwili wa aliyekua mlinzi wa Bonite.
Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo la mauaji wakishangaa mwili wa aliyekua mlinzi wa Bonite. 
Mlinzi wa Bonite akiwa ameshikilia bunduki yake aina ya Short Gun, muda mfupi baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walifanikiwa kupora fedha. 

Tarehe 20/04/2015, majira ya saa 12 jioni, katika eneo la Soweto ya chini eneo la Radio Kli Fm, Kata ya Soweto, Tarafa ya Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi, gari la Bonite lenye usajili wa namba T.803 ATR aina ya Toyota Hiace lililotoka kwenye makusanyo ya fedha za mauzo lilivamiwa na majambazi wapatao wanne waki na Bastola huku wakitumia usafiri wa pikipiki mbili aina ya Boxer na Srm.

Katika tukio hilo mtu aitwaye Edson Shamba(56), Mnyirambamkazi wa matindigani ambaye alikua ni mlinzi na alikua akisindikiza gari hilo akiwa na bunduki aina ya Short Gun namba 8710653 ikiwa na risasi tano aliuwawa papo hapo kwa kupigwa risasi maeneo ya kichwa, ambapo Amini Mselemu(61), Mnyao, mkazi wa mtaa wa Chunya Moshi aliyekua dereva wa gari hiyo, alipigwa risasi maeneo ya kifuani, tumboni, mkononi na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu usiku wa jana katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.

Miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC mjini Moshi na jeshi la polisi linaendelea na kuwatafuta wahusika ili kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment