Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, April 21, 2015

Mbunge wa jimbo la Siha ambaye ni Naibu waziri wa TAMISEMI apata pigo la kisiasa


KILIMANJARO Mbunge wa Jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro (CCM), ambaye pia ni Naibu waziri wa serikali za mikoa na tawala  za Mitaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),amepata pigo la kisiasa baada ya Msomi mwenye taaluma ya Uchumi Paulo Mongi (CHADEMA), kujitokeza kugombea jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
 Mongi ametangaza nia hiyo juzi mbele ya waaandishi wa habari mjini hapa na kuongeza atagombea jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kumshinda Mwanri ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa vipindi vitatu mfululizo kupitia tiketi ya CCM.

Mchumi huyo amesema amefikia uamuzi huo kutokana na mfumo wa siasa wa sasa unavyotawala  hauwasaidii wananchi kuwa wamiliki wa vyanzo vya uzalishaji mali hususani wananchi wa tabaka la chini kama wakulima,wafugaji na wavuvi.
Amesema asimia kubwa ya wakazi wa jimbo la Siha ni wakulima na wafugaji, lakini changamoto kubwa kwao wananchi hao hawapati fursa ya kumiliki thamani ya mazao yao hivyo endapo atapata fursa hiyo atahakikisha anawaunganisha katika fursa za kumiliki mazao na biashara zao kiuchumi na hivyo kuwapunguzia kama si kumaliza umasikini unaowakabili.

Mongi ameeleza kuwa kupitia taaluma yake atahakikisha anapeleka mageuzi ya kiuchumi katika jimbo la Siha ili wananchi hao waweze kunufaika na mazo yao ambayo mengi wamekuwa hawapati faida kutokana na kutokuwepo na kiongozi wa kuwaunganisha katika masoko.

Katika hatua nyingine Mongi amesema kuwa kupitia taaluma yake hiyo atawawezesha wakulima kuwaunganisha na Chama cha wakulima wa Maembe (AMAGRO), kwani Tanzania imepata soko kubwa kutoka nchi ya Saud Arabia , lakini kutokana na wakulima kutokuwezeshwa  wamekuwa katika hali duni ya kimaisha.

No comments:

Post a Comment