Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 17, 2015

UN KUSAFISHA KILIMANJARO


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkaribisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo.

Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez, alikutana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na kufanya naye mazungumzo.

Miongoni mwa mambo waliyojadili ni maandalizi ya shughuli na matukio kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa (UN@70 ).

Katika mazungumzo yao walikubaliana kufanya shughuli ya upandaji miti kuzunguka Mlima Kilimanjaro na kusafisha sehemu ya mji kabla ya Siku ya Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa mkoa alikubaliana na wazo hilo na kusema shughuli hiyo inafaa kufanyika katikati ya mwezi wa Agosti 2015.

Wawili hao wakipiga picha ya pamoja.

Wakiagana.

No comments:

Post a Comment