Katika hali isyokuwa ya kawaida leo Bunge limelipuka kwa furaha kubwa sana pale Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa analiaga na kulivunja bunge alipompongeza kwa mema aliyoyafanya mgombea wa sasa wa Urais Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowasa. Hali hiyo imewaacha watabiri wa siasa nchini kubaki solemba na kinachokuja kwenye mchujo wa wagombea huko ndani ya CCM Dodoma sasa hivi.
Waziri mkuu wa zamani Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amelitikisa baada ya Rais Jakaya Kikwete kumpongeza kwa kazi nzuri alioifanya kwa kipindi cha miaka miwili wakati akiwa Waziri mkuu.
Mara baada ya Lowassa kutajwa ukumbi mzima wa Bunge ulilipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo hali iliyopelekea hotuba ya Rais Kikwete kusimama kwa sekunde 53 hali iliyomlazimu Lowassa kusimama na kutoa heshima kwa wabunge.
Rais Kikwete alisikika akisema "katika kipindi kifupi alichokuwa Waziri Mkuu amefanya kazi nzuri". Ukumbi ukazidi kulipuka kwa shangwe. Shangwe zile kwa Lowassa ni ishara ya kubaliko la utumishi uliotukuka aliouonyesha na JK kumpa stahiki yake.
Mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia. Lowassa ni kiongozi mwenye haiba ya kupendwa na kukubalika zaidi kwa watu.
No comments:
Post a Comment