Hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro, inayomilikiwa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania (KKKT) imeanza kufanyiwa upanuzi wa majengo yake ili kuondoa changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na uchache wa majengo hususani kitengo cha upasuaji na kitengo cha dharura.
Kaimu mkurungenzi mkuu wa KCMC Profesa Raimos Olomi, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema upanuzi huo utasaidia kuboresha zaidi huduma za
kitabibu zitolewazo katika hospitali hiyo, ambayo
ina zaidi ya miaka arobaini tangu ilipojengwa.
Dokta Giliarld
Masenga, ambaye ameteuliwa na bodi ya KCMC kushika nafasi ya mkurugenzi
mkuu wa hospitali hiyo alisema kipaumbele chake ni kushawishi uongozi wa hospitali kuongeza idadi ya
watumishi ili kuondoa upungufu wa madaktari na wauguzi uliopo katika hospitali
hiyo ambapo idadi ya wagonjwa imekuwa
ikiongezeka kwa kiwango kikubwa.
No comments:
Post a Comment