Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 17, 2015

MWANAMUZIKI BANZA STONE AFARIKI DUNIA

 Banza Stone enzi za uhai wake

MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Dansi nchini, Ramadhani Masanja "Jenerali Banza Stone " amefariki Dunia hivi punde nyumbani kwao Mtaa wa Sinza D, Dar Es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu na hivi sasa mwili wake unapelekwa kufadhiwa Hospitali.
Sisi watoto tuliokuwa na Banza Kata ya Sinza Dar Es Salaam, tuliishi vyema na Banza Kabla ajaanza kuugua na hadi alivyoumbukwa NA Maradhi.
Binafsi siku zote uwa name heshimu kubwa Banza pamoja na mapungufu yake ya kibo adabu ambayo yalisababisha Katika Uhai wake ajiingize Kutenda baadhi ya matendo Katika Jamii ambayo hayakutupendeza sisi wana Sinza wenzake na mashabiki wake wa muziki.
Daima Nitamkumbuka Banza,kwasababu Banza ni miongoni mwa watu mahususi walioshiriki kuitaka Kata ya Sinza kupitia taaluma yake ya muziki Kwani baadhi ya Nyimbo zake alikuwa alitaja sana eneo la Sinza Hali iliyosababisha eneo la Sinza Kuwa ni eneo maarufu sana.
Banza alikuwa ni rafiki mkubwa wa Kaka yangu Liston Mwesiga Katabazi.

Banza ulishindwa kwenda sambamba na Maudhuhi ya Wimbo wako wa KUMEKUCHA. Ndani ya Wimbo huo kuna maneno yake mayo 'Unapotaka kuanza Maisha Anza sasa usisubiri Kesho Kwani Utamkuta Mwana siwako Oooh,upatapo fahamu Jua Umepotea kweli Umepotea.
Wimbo huo naupenda sana kuliko Nyimbo zake zote aliziwahi kuimba Banza.

Pole familia ya Banza na wapenzi wa muziki wa dansi na wakazi wenzangu wote tunaoshi Kata ya Sinza .
Mungu aiweke roho yake mahali pana postahili.

Na Happiness Katabazi,

No comments:

Post a Comment