MJUMBE wa Halmashaurishauri Kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa NEC, Wilaya ya Siha Meijo Laizer, amesema kwa sasa hatagombea nafasi ya Ubunge wa jimbo la Siha kama alivyotangaza awali. Hatua hiyo imekuja baada ya kuombwa kufanya hivyo na viongozi mbalimbali wakiwamo wa Chama na mila.
Akizungumza na vyombo waandishi wa habari leo, alisema kuwa kwa sasa hatagombea nafasi hiyo kama alivyotangaza awali, nafasi ambayo inashikiliwa na Aggrey Mwandri ambaye ni Naibu waziri wa Tamisem.
Leizer alisema kuwa sababu ya yeye kutogombea nafasi hiyo ni kutokana na ombi la Wazee wa CCM wa Wilaya hiyo ya kutaka kumuachia nafasi hiyo Aggrey Mwandri, kwani amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu Taifa NEC, alitaja sababu ya pili ni Viongozi wa kimila Jamii ya Wafugaji Olgwanani, ambao walimfuata na kumtaka asigombee nafasi hiyo hadi muda wake utakapo fika, kwa sasa tumuachie Mh. Aggrey Mwandri, amalizie muda uliosalia wa miaka mitano walisema viongozi hao.
Mjumbe huyu alisema, Binafsi nimekubaliana na ombi hilo na hii ni heshima kwa chama chetu, kwani umoja wetu unaendelea kuwa imara zaidi, umoja wetu tutapata ushindi wa kishindo kwa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais.
No comments:
Post a Comment