Mkurugenzi idara ya uratibu wa maafa ofisi ya waziri mkuu Bregedia Jenerali Mbalizi Msuya ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa idara za kilimo katika wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro
kuhusu umuhimu wa kukubaliana na athari za majanga na maafa kabla ya kuleta madhara makubwa kwa wananchi.
Amesema tayari serikali imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na athari hizo kwa kuanzisha miradi hiyo kwa wananchi waliokumbwa na ukame katika wilaya za mikoa ya Kilimanjaro na Shinyanga pamoja na kutoa elimu ya kulima mazao ya muda mfupi na yanayohimili ukame.
Kwa upande wake katibu tawala mkoa Kilimanjaro Bwana Severine Kahitwa amesema kutokana na mkoa kukumbwa na janga la ukame na mafuriko mwaka huu katika wilaya za Hai, Mwanga, Moshi na Same umesababisha wananchi kukosa mavuno na hivyo mkoa wa Kilimanjaro kwa sasa unahitaji chakula cha msaada zaidi ya tani 9000.
Mratibu wa maafa wilaya ya Same ambapo mradi huo wa majaribio wa kusaidia wananchi umeanza Bwana Ally Mmbwaya, amesema jiografia ya wilaya hiyo asilimia 70 ni milima na kwamba wameelekeza elimu kwa wananchi kuachana na kilimo cha mahindi na badala yake walime mazao kama mtama na mihogo ambayo hustaimili ukame.
No comments:
Post a Comment