Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 14, 2015

Waislamu Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelea kufanya yaliyo mema


Image result for mwezi mtukufu wa ramadhani
KILIMANJARO zikiwa zimebaki siku chache kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Waislamu  Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelea kufanya yaliyo mema ili kumalizia Mfungo huo.

Akizungumza na waumini hao mara baada ya kuswali Sala ya dhuhuri Msikiti wa Sanya juu Immam Ali Muhamedi, alisema kuwa huu ni muda ambao Waislamu wanapaswa kujipendekeza kwa Mola hasa kwa kufanya mema.

Muhamedi alisema kuwa zimesalia siku chache katika kumi la mwisho ni lazima Waislamu wakahakikisha wanasoma QURUAN na pia wanatoa misaada kwa watu mbalimbali hasa kwa watu wasiojiweza.

Alise tupo kumi la mwisho wengine wanafurahi kumaliza mwezi huu Mtukufu, lakini lazima tuutumie kwani ni mwezi ambao umechaguliwa mara mmoja kwa mwaka.

Pia amewata waislamu kujiandaa kwa kutoa zaka kwani hayo ndiyo maamrisho ya dini na Mtume Muhamad[S.A.W]

No comments:

Post a Comment