Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, May 3, 2017

MEIMOSI: KAMPUNI YA PANONE YAWA KIVUTIO NA SHELI INAYOTEMBEA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli
Akiwapungia mkono wafanyakazi wa Panone and Company ltd wakati wakipita
mbele yake kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi mjini Moshi. 


Kila tarehe 01/05 maarufu kama Mei Mosi ni siku ku ya wafanyakazi Duniani, Katika siku hii mataifa mbalimbali duniani huazimisha siku hii kubwa ya wafanyakazi kwa kufanya sherehe ambazo hukutanisha wafanyakazi pamoja na kujadili changamoto mbalimbali ikiwa ni sehemu pekee ya kueleza serikali changamoto zao zinazowakabili.

Kwa upande wa Tanzania sikukuu ya Mei mosi kitaifa imefanyika katika Viwanja vya Ushirika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Taasisi na Makampuni mbalimbali zilishiriki maadhimisho hayo ambayo yaliongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli huku akiongozana na Makamu wa Rais Mh. Samiah Suluhu na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.

Gari za zinazotoa huduma za Panone zikiwa katika maandamano ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei mosi.


Katika maadhimisho hayo yapo makampuni na taasisi mbalimbali yaliyokua kivutio huku yakionesha ufanisi na bidhaa zao. Moja ya kampuni zilizokua kivutio ni kampuni ya Panone and Co. Ltd. Ubunifu na aina ya uwasilishaji wao ulikua kivutio na walitambulisha huduma ambayo imeonekana kama kivutio na msaada kwa jamii. Hukuma ya Uuzwaji wa mafuta kwa gari maalum inayomfuata mteja (Mobile Petrol Station) Akizungumza na Mwandishi wetu Meneja wa kampuni ya Panone Ndugu Gido Marandu alisema kutokana na changatizamoto mbalimbali zinazowakabili wamiliki wa vyombo vya usafiri na taasisi mbalimbali kuhusu ununuaji wa mafuta na wakati mwingine wanashindwa kufika kituo cha mafuta na kupelekea kupata tatizo la kuishiwa mafuta Panone imeona ni wasaa sasa wa kuweza kuwafikia wateja walipo na kuwa msaada kwao.

Wafanyakazi wa Panone wakiwa katika Maandamano ya maadhimizho ya siku kuu ya wafanyakazi Mei mosi.


Akizungumzia gharama za huduma hii Marandu alisema huduma hii ya kuletewa mafuta ulipo kwa gari iisyo na utofauti na kituo cha mafuta kwa kuwa ina Digital pump kama ya kituoni hakuna gharama ya ziada na mteja atalipia bei elekezi ya mafuta iliyoelekezwa na serikali na Zaidi ya yote atapata punguzo la bei la shilingi hamsini (50) kwa kila lita moja atakayonunua hii ikiwa ni tofauti ya bei ya kituoni.
Moja ya njia ya kufikisha ujumbe ni kwa njia ya maandishi kwenye mabango, Wafanyakazi wa Panone
wakiwa na mabango yenye ujumbe katika maandamano.


Pia Marandu aliweza kuelezea baadhi ya huduma za Panone alielezea Uwepo wa Kampuni ya Ngiloi Ulomi Enterprises ambayo inajihusisha na uuzaji wa Oil za Magari, Tairi za Magari na kutoa huduma ya matengenezo ya Magari ambapo huduma hizo zipo katika vituo vyote vya Panone Tanzania nzima. Mbali na hilo aliweza kueleza uwepo wa Panone Hotels, Hizi ni hotel za Panone ambazo zipo maeneo mbalimbali huku akizungmzia Hotel ya Panone  Garden Hotel iliyopo Sakina kwa Idi ambayo awali ilikua ikifahamika kama 4js Hotel na Hotel ya Panone Luxury Motel iliyopo king’ori. Pia Kampuni ya Panone inatoa huduma ya uuzaji wa kuku wa nyama, Pamoja na uuzaji wa mayai ya kuku kupitia Panone Poutry na kwa mahitaji ya Mikate, Cake, Crips za Panone na maandazi bidhaa mbalimbali na bbasi tembelea Supermarket za Panone zilizopo katika Vituo vyote vya Panone na zinafanya kazi kwa saa Ishirini nan ne za siku (24.) “Ni wasaa wa wateja wetu kupata huduma toka Panone na kutoa mapendekezo yao kwetu jinsi ya kuboresha huduma zetu” Alisema Marandu.

Wafanyakazi wa Panone wakiingia Uwanja wa Ushirika kwenye kilele cha Sherehe za Mei mosi.


Alipoulizwa juu ya Matarajio ya Panone Marndu alisema huu ni wakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma Bora, Mteja kwetu ni mtu wa kwanza katka Huduma, Ili tuweze kupata faida ni lazima tuwe na wateja. Na ili kuongeza wateja ni lazima tuwe na huduma bora kwa kuwa mteja ndio analeta mteja tumejizatiti kuwa na huduma bora ili kuongeza wateja. Na pia tukiwa na malengo wa kuenea maeneo mengi ili kuwapa wananchi huduma na hivi karibuni tunatarajia kufungua kituo kikubwa pale chekereni ya Kilewo njia ya kuelelea Dar es salaam kutokea Moshi nah ii ni moja ya malengo yetu makuu ya kusogeza huduma karibu kwa jamii.

Uvivu hauna nafasi katika nchi yetu, Hapa kazi tu.



Alimaliza kwa kuongelea kuhusu Sherehe za Meimosi na wafanyakazi huku akisema Panone inawajengea uwezo wafanyakazi kuweza kujituma kazini na kujijengea msingi imara wa maisha yao ya sasa naya baadae. Ili kampuni iendelee kuwepo na ajiri iendelee kuwepo ni vyema wakajituma kazini na kumuheshimu mteja hii itawezesha kampuni kupata faida na kuboresha maslahi yao mara kwa mara na pia kutengeneza ajira mpya za watu wengine kupitia uzalishaji unaoanzia kwao.

Wafanyakazi wa Panone wakipita mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli katika sherehe za Mei mosi.

No comments:

Post a Comment