Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Bw. Augustino Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya
awamu
ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo
hayo ya awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja
kati ya TADB, NABAD na MIVARF.
Meneja
Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya
kufanyia uchambuzi miradi ya kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa
mikopo
kwenye sekta hiyo.
Washiriki
wa Mafunzo ya Awamu ya Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo
wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi na viongozi kutoka TADB.
Na mwandishi wetu,
Mabenki yameombwa kuwa tayari kukopesha mnyonyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga mkono juhudi
za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Hayo
yamesemwa na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha wakati
akifungua mafunzo ya
awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo
yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya
Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu
ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za
Kifedha Vijijini (MIVARF).
Bw.
Chacha amesema kuwa mabenki na taasisi za kifedha nchini hazina budi
kuwekeza mtaji wa kutosha ili kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni
uti wa mgongo
wa Tanzania na ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo
wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya
asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
Ameongeza
kuwa kuanzinshwa kwa TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara
kupata fedha zenye masharti nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta
ya kilimo
ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
“Hakuna
haja ya kuogopa kukopesha sekta ya kilimo kwani ni sekta yenye umuhimu
mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, TADB kama benki kiongozi
ya maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi
nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa kilimo,
imejipanga kusaidia upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu na
endelevu, ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo katika
mfumo wa kifedha,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda
kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza sekta ya kilimo TADB imejipanga uwa
benki ya
mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji
wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Bw. Kamanda ameongeza kuwa TADB imejipanga kupunguza changamoto za ukopeshaji zinazoikabili sekta ya kilimo nchini.
No comments:
Post a Comment