Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Monday, March 12, 2018

SHIRIKA LA AGPAHI LAANZA KAMBI YA WATOTO NA VIJANA YA WIKI MOJA MJINI MOSHI – MKOANI KILIMANJARO

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akiwa katika picha ya Pamoja na Vijana na Watoto Nje ya Ukumbi wa hotel ya Uhuru iliyopo Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. 
Toka mwaka 2011 Shirika la Arial Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)  Iimekua Msaada mkubwa kwa watoto wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Tanzania. Shirika hili la kimataifa lisilo la Kiserikali lilianzishwa kwa Msaada wa Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation  (EGPAHI) huku lengo kuu likiwa kutokomeza Ukimwi kwa watoto  nchini Tanzania. Mpaka sasa ni Takribani Miaka saba Shirika hili limekua Msaada mkubwa kwa watoto hao wanaoishi na VVU kutimiza Ndoto zao.

Watoto na Vijana wakimpokea Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita Katika Ufunguzi wa Kambi ya vijana na watoto Mapema  leo Mjini Moshi.

Kila Mwaka Shirika la AGPAHI huandaa Kambi ya watoto kutoka katika Mikoa sita inayofanya kazi nayo ambayo ni Mikoa ya Tanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Mara na Shinyanga. Kambi hiyo hukusanya watoto kutoka katika vikundi vya watoto na vijana ambavyo huundwa katika Vituo vya Afya husika. Watoto hao huudhuria katika vikundi ili kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa tiba na elimu kuhusu matumizi sahihi ya Dawa za Kupungua Maambukizi ya VVU (ARV’s). Vikundi hivyo huwezeshwa kwa msaada wa shirika la AGPAHI kwa msaada wa watu wa Marekani.  Kupitia vikundi watoto na vijana hupata fursa ya kuhudhuria kambi ya wiki moja inayoandaliwa na shirika la AGPAHI. 

Mgeni Rasmi aliwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na Uongozi,Madaktari na wataalamu wa masuala ya watoto nje ya ukumbi wa hoteli ya Uhuru mjini Moshi.

Leo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga   Dr. Asha Mahita amefungua Kambi ya wiki moja ya watoto na vijana katika Ukumbi wa Hotel ya Uhuru  Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Dr. Mahita alitumia nafasi hiyo kuzungumza moja kwa moja na watoto takribani hamsini (50) kutoka Mikoa mitatu ya Tanga, Mwanza na Geita ambao wamehudhuria kambi hiyo. Watoto na vijana wenye umri wa miaka 10 – 17.

“Fursa hii kwangu ni fursa hadimu sana kukutana na watoto wengi kama ninyi wenye tumaini kuu na hari ya kutimiza ndoto, Nawahakikishia kuwa siku moja mtasimama na kuidhihirishia jamii kwa vitendo kuwa mnaweza, Cha muhimu ni kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuendelea kuwepo kwenye huduma.” Alisema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Dr. Mahita akijibu swali la mmoja wa watoto waliomuuliza maswali leo.

Pia aliweza kukaa na watoto na kuzungumza nao kuhusu afya zao na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali  kuhusu ufahamu wa  VVU / UKIMWI kitaalamu. Moja ya maswali hayo ni:- Njia za Maambukizi ya VVU, Faida ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU.

Watoto na vijana wakiuliza maswali kwa Mgana Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Mahita.


Hata hivyo AGPAHI waliweza kueleza dhumuni kuu la kambi hiyo Kuwakutanisha watoto na vijana ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu afya, Kutoa ushauri wa  Kisaikolojia kwa watoto wanaoishi na VVU, lakini pia kuwasaidia uangalizi wa afya zao na maendeleo ya afya zao. Ambapo katika kambi hii kuna Mtaalamu wa Saikolojia ambaye wakati wote wa kambi atatoa nafasi ya kuzungumza na kila mtoto kwa wakati wake ili kuweza kufahamu na kutatua yale ambayo yanawakabili kitaalamu. Lakini pia katika kambi hii kuna Madaktari Bingwa wa watoto  ambao wakati wote watakua wakiwahudumia watoto katika kipindi chote cha kambi.

Meneja mawasiliano Bi. Jane Shuma akielezea Dhumuni la Kambi ya vijana na watoto katika sherehe za ufunguzi wa kambi ya wiki moja mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.


 AGPAHI wanaamini watoto kujifunza katika michezo ni moja ya Eneo sahihi hivyo basi  wamewashirikisha wawezeshaji wa Michezo ambao wameandaa mpango maalumu wa mafunzo kupitia Michezo kwa siku zote za kambi hiyo.

Mtoto akicheza katika kipindi cha elimu kwa njia ya Michezo.
Pia watoto walipata fursa ya kusikia machache na kuuliza maswali kutoka kwa Kijana Muelimishaji rika kutoka Mwanza ambaye ameshahudhuria  Kambi kadhaa za vijana. Muelimishaji rika huyo alieleza faida ya mafunzo ya kambi, ambayo ni kuweza kupata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa Vijana wa Dunia huku yeye akiwakilisha Vijana wa Afrika.  “Nilihudhuria Mafunzo mwaka 2013, Nilifundishwa kujiamini na kuijua thamani yangu, Mafunzo haya yameniwezesha kuaminika na kuiona Thamani yangu.” Alisema  Muelimisha Rika.


Mtoto akiuliza swali kwa kijana Muelimishaji Rika baada ya kuzungumza na kuruhusu maswali.

“Moja ya changamoto Shirika inazokabiliana nazo ni watoto wengi waliozaliwa na VVU kujinyanyapaa na kutokubali hali ya kuishi maambukizi. Hii hupelekea kutokutumia dawa kwa usahihi, kupata magonjwa nyemelezi na kupelekea kifo, Changamoto nyingine ni jamii kuendeleza unyanyapaa na Ubaguzi kwa watoto…..ubaguzi  ambao hupelekea watu wanaoishi na VVU kujinyanyapaa wenyewe na kuona kwamba hawahitajiki kwenye jamii ndio maana shirika la AGPAHI linafanya kazi kwa karibu na wahudumu wa afya ili waweze kuwasaidia watoto  kutumia dawa kwa usahihi na kwa wakati pamoja na  kuhudhuria Kliniki  kila mwezi kama inavyoshauriwa” Alisema Jane Shuma Meneja Mawasiliano - AGPAHI



Wednesday, May 3, 2017

MEIMOSI: KAMPUNI YA PANONE YAWA KIVUTIO NA SHELI INAYOTEMBEA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli
Akiwapungia mkono wafanyakazi wa Panone and Company ltd wakati wakipita
mbele yake kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi mjini Moshi. 


Kila tarehe 01/05 maarufu kama Mei Mosi ni siku ku ya wafanyakazi Duniani, Katika siku hii mataifa mbalimbali duniani huazimisha siku hii kubwa ya wafanyakazi kwa kufanya sherehe ambazo hukutanisha wafanyakazi pamoja na kujadili changamoto mbalimbali ikiwa ni sehemu pekee ya kueleza serikali changamoto zao zinazowakabili.

Kwa upande wa Tanzania sikukuu ya Mei mosi kitaifa imefanyika katika Viwanja vya Ushirika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Taasisi na Makampuni mbalimbali zilishiriki maadhimisho hayo ambayo yaliongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli huku akiongozana na Makamu wa Rais Mh. Samiah Suluhu na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.

Gari za zinazotoa huduma za Panone zikiwa katika maandamano ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei mosi.


Katika maadhimisho hayo yapo makampuni na taasisi mbalimbali yaliyokua kivutio huku yakionesha ufanisi na bidhaa zao. Moja ya kampuni zilizokua kivutio ni kampuni ya Panone and Co. Ltd. Ubunifu na aina ya uwasilishaji wao ulikua kivutio na walitambulisha huduma ambayo imeonekana kama kivutio na msaada kwa jamii. Hukuma ya Uuzwaji wa mafuta kwa gari maalum inayomfuata mteja (Mobile Petrol Station) Akizungumza na Mwandishi wetu Meneja wa kampuni ya Panone Ndugu Gido Marandu alisema kutokana na changatizamoto mbalimbali zinazowakabili wamiliki wa vyombo vya usafiri na taasisi mbalimbali kuhusu ununuaji wa mafuta na wakati mwingine wanashindwa kufika kituo cha mafuta na kupelekea kupata tatizo la kuishiwa mafuta Panone imeona ni wasaa sasa wa kuweza kuwafikia wateja walipo na kuwa msaada kwao.

Wafanyakazi wa Panone wakiwa katika Maandamano ya maadhimizho ya siku kuu ya wafanyakazi Mei mosi.


Akizungumzia gharama za huduma hii Marandu alisema huduma hii ya kuletewa mafuta ulipo kwa gari iisyo na utofauti na kituo cha mafuta kwa kuwa ina Digital pump kama ya kituoni hakuna gharama ya ziada na mteja atalipia bei elekezi ya mafuta iliyoelekezwa na serikali na Zaidi ya yote atapata punguzo la bei la shilingi hamsini (50) kwa kila lita moja atakayonunua hii ikiwa ni tofauti ya bei ya kituoni.
Moja ya njia ya kufikisha ujumbe ni kwa njia ya maandishi kwenye mabango, Wafanyakazi wa Panone
wakiwa na mabango yenye ujumbe katika maandamano.


Pia Marandu aliweza kuelezea baadhi ya huduma za Panone alielezea Uwepo wa Kampuni ya Ngiloi Ulomi Enterprises ambayo inajihusisha na uuzaji wa Oil za Magari, Tairi za Magari na kutoa huduma ya matengenezo ya Magari ambapo huduma hizo zipo katika vituo vyote vya Panone Tanzania nzima. Mbali na hilo aliweza kueleza uwepo wa Panone Hotels, Hizi ni hotel za Panone ambazo zipo maeneo mbalimbali huku akizungmzia Hotel ya Panone  Garden Hotel iliyopo Sakina kwa Idi ambayo awali ilikua ikifahamika kama 4js Hotel na Hotel ya Panone Luxury Motel iliyopo king’ori. Pia Kampuni ya Panone inatoa huduma ya uuzaji wa kuku wa nyama, Pamoja na uuzaji wa mayai ya kuku kupitia Panone Poutry na kwa mahitaji ya Mikate, Cake, Crips za Panone na maandazi bidhaa mbalimbali na bbasi tembelea Supermarket za Panone zilizopo katika Vituo vyote vya Panone na zinafanya kazi kwa saa Ishirini nan ne za siku (24.) “Ni wasaa wa wateja wetu kupata huduma toka Panone na kutoa mapendekezo yao kwetu jinsi ya kuboresha huduma zetu” Alisema Marandu.

Wafanyakazi wa Panone wakiingia Uwanja wa Ushirika kwenye kilele cha Sherehe za Mei mosi.


Alipoulizwa juu ya Matarajio ya Panone Marndu alisema huu ni wakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma Bora, Mteja kwetu ni mtu wa kwanza katka Huduma, Ili tuweze kupata faida ni lazima tuwe na wateja. Na ili kuongeza wateja ni lazima tuwe na huduma bora kwa kuwa mteja ndio analeta mteja tumejizatiti kuwa na huduma bora ili kuongeza wateja. Na pia tukiwa na malengo wa kuenea maeneo mengi ili kuwapa wananchi huduma na hivi karibuni tunatarajia kufungua kituo kikubwa pale chekereni ya Kilewo njia ya kuelelea Dar es salaam kutokea Moshi nah ii ni moja ya malengo yetu makuu ya kusogeza huduma karibu kwa jamii.

Uvivu hauna nafasi katika nchi yetu, Hapa kazi tu.



Alimaliza kwa kuongelea kuhusu Sherehe za Meimosi na wafanyakazi huku akisema Panone inawajengea uwezo wafanyakazi kuweza kujituma kazini na kujijengea msingi imara wa maisha yao ya sasa naya baadae. Ili kampuni iendelee kuwepo na ajiri iendelee kuwepo ni vyema wakajituma kazini na kumuheshimu mteja hii itawezesha kampuni kupata faida na kuboresha maslahi yao mara kwa mara na pia kutengeneza ajira mpya za watu wengine kupitia uzalishaji unaoanzia kwao.

Wafanyakazi wa Panone wakipita mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli katika sherehe za Mei mosi.