Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akiwa katika picha ya Pamoja na Vijana na Watoto Nje ya Ukumbi wa hotel ya Uhuru iliyopo Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. |
Toka mwaka 2011 Shirika la Arial Glaser Pediatric AIDS
Healthcare Initiative (AGPAHI) Iimekua
Msaada mkubwa kwa watoto wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Tanzania.
Shirika hili la kimataifa lisilo la Kiserikali lilianzishwa kwa Msaada wa
Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation
(EGPAHI) huku lengo kuu likiwa kutokomeza Ukimwi kwa watoto nchini Tanzania. Mpaka sasa ni Takribani Miaka
saba Shirika hili limekua Msaada mkubwa kwa watoto hao wanaoishi na VVU
kutimiza Ndoto zao.
Watoto na Vijana wakimpokea Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita Katika Ufunguzi wa Kambi ya vijana na watoto Mapema leo Mjini Moshi. |
Kila Mwaka Shirika la AGPAHI huandaa Kambi ya watoto kutoka katika Mikoa sita inayofanya kazi nayo ambayo ni Mikoa ya Tanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Mara na Shinyanga. Kambi hiyo hukusanya watoto kutoka katika vikundi vya watoto na vijana ambavyo huundwa katika Vituo vya Afya husika. Watoto hao huudhuria katika vikundi ili kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa tiba na elimu kuhusu matumizi sahihi ya Dawa za Kupungua Maambukizi ya VVU (ARV’s). Vikundi hivyo huwezeshwa kwa msaada wa shirika la AGPAHI kwa msaada wa watu wa Marekani. Kupitia vikundi watoto na vijana hupata fursa ya kuhudhuria kambi ya wiki moja inayoandaliwa na shirika la AGPAHI.
Mgeni Rasmi aliwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na Uongozi,Madaktari na wataalamu wa masuala ya watoto nje ya ukumbi wa hoteli ya Uhuru mjini Moshi. |
Leo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita amefungua Kambi ya wiki moja
ya watoto na vijana katika Ukumbi wa Hotel ya Uhuru Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Dr. Mahita
alitumia nafasi hiyo kuzungumza moja kwa moja na watoto takribani hamsini (50)
kutoka Mikoa mitatu ya Tanga, Mwanza na Geita ambao wamehudhuria kambi hiyo. Watoto
na vijana wenye umri wa miaka 10 – 17.
“Fursa hii kwangu ni fursa hadimu sana kukutana na watoto
wengi kama ninyi wenye tumaini kuu na hari ya kutimiza ndoto, Nawahakikishia
kuwa siku moja mtasimama na kuidhihirishia jamii kwa vitendo kuwa mnaweza, Cha
muhimu ni kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuendelea kuwepo kwenye huduma.”
Alisema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Dr. Mahita akijibu swali la mmoja wa watoto waliomuuliza maswali leo. |
Pia aliweza kukaa na watoto na kuzungumza nao kuhusu afya
zao na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali kuhusu ufahamu wa VVU / UKIMWI kitaalamu. Moja ya maswali hayo
ni:- Njia za Maambukizi ya VVU, Faida ya kutumia dawa za kupunguza makali ya
VVU.
Watoto na vijana wakiuliza maswali kwa Mgana Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Mahita. |
Hata hivyo AGPAHI waliweza kueleza dhumuni kuu la kambi hiyo
Kuwakutanisha watoto na vijana ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu afya,
Kutoa ushauri wa Kisaikolojia kwa watoto
wanaoishi na VVU, lakini pia kuwasaidia uangalizi wa afya zao na maendeleo ya afya
zao. Ambapo katika kambi hii kuna Mtaalamu wa Saikolojia ambaye wakati wote wa kambi
atatoa nafasi ya kuzungumza na kila mtoto kwa wakati wake ili kuweza kufahamu
na kutatua yale ambayo yanawakabili kitaalamu. Lakini pia katika kambi hii kuna
Madaktari Bingwa wa watoto ambao wakati
wote watakua wakiwahudumia watoto katika kipindi chote cha kambi.
Meneja mawasiliano Bi. Jane Shuma akielezea Dhumuni la Kambi ya vijana na watoto katika sherehe za ufunguzi wa kambi ya wiki moja mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. |
AGPAHI wanaamini
watoto kujifunza katika michezo ni moja ya Eneo sahihi hivyo basi wamewashirikisha wawezeshaji wa Michezo ambao
wameandaa mpango maalumu wa mafunzo kupitia Michezo kwa siku zote za kambi
hiyo.
Mtoto akicheza katika kipindi cha elimu kwa njia ya Michezo. |
Mtoto akiuliza swali kwa kijana Muelimishaji Rika baada ya kuzungumza na kuruhusu maswali. |
“Moja ya changamoto Shirika inazokabiliana nazo ni watoto
wengi waliozaliwa na VVU kujinyanyapaa na kutokubali hali ya kuishi maambukizi.
Hii hupelekea kutokutumia dawa kwa usahihi, kupata magonjwa nyemelezi na kupelekea
kifo, Changamoto nyingine ni jamii kuendeleza unyanyapaa na Ubaguzi kwa watoto…..ubaguzi
ambao hupelekea watu wanaoishi na VVU
kujinyanyapaa wenyewe na kuona kwamba hawahitajiki kwenye jamii ndio maana
shirika la AGPAHI linafanya kazi kwa karibu na wahudumu wa afya ili waweze
kuwasaidia watoto kutumia dawa kwa
usahihi na kwa wakati pamoja na
kuhudhuria Kliniki kila mwezi kama
inavyoshauriwa” Alisema Jane Shuma Meneja Mawasiliano - AGPAHI
No comments:
Post a Comment