Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 27, 2012

Kiongozi wa Mgomo wa Madaktari Dr Ulimboka akutwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana



                                     Dr. Steve Ulimboka

 Jana usiku Dr. Ulimboka alikuwa akiongea na Dr. mwenzake na mtu mwingine ambaye inasemekana anayefanya kazi ikulu. Wakati wakiendelea na mazungumzo ambayo lengo la mazungumzo hayo ni kuzungumzia mgomo wa madaktari unaoendelea nchini Tanzania. Punde wakatokea watu wasiojulikana na kumwabia Dr. Ulimboka kuwa yupo chini ya ulinzi na walimchukua na kumuingiza kwenye gati lisilokuwa na namba na kumpeleka pasipojulikana, Juhudi za kumtafuta Dr. Ulimboka liendelea kwa kumtafuta kwenye vituo vya polisi bila mafanikio yoyote ila leo asubui taarifa kutoka kwa wasamaria wema ilibaini kuwa Dr. Ulimboka yupo Mabwe pande na juhudi za kuelekea magu pande zilianza ambapo ndugu jamaa na marafiki walimkuta Dr. Ulimboka akiwa kwenye hali mbaya sana maana alikuwa amepigwa na kuumizwa sana, alikuwa akitokwa damu mwili mzima na sehemu ya machoni, Dr. Uliomboka alilalamika na kusema anahisi kuishiwa nguvu na kuomba msaada wa maji, ndipo alipo chukuliwa na kupelekwa hospital ya muhimbili kwa matibabu zaidi. Mpaka sasa Dr. Ulimboka yupo hospitali ya muhimbili..
Tutaendelea kukujuza kuhusu nini kinaendelea kuhusu Dr. Steve Ulimboka.

No comments:

Post a Comment