Wamama wajawazito wakisubiria muafaka wa mgomo wa madaktari
MADKTARI katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro wametangaza mgomo mkali
kuliko sikuzote kufuatia kukamatwa na kupigwa kwa kiongozi wa chama cha
madaktari nchi Dr. Steven Ulimboka.
Wakizungumza mara baada ya kupita katika wodi zote
wakiwatoa madaktari waliokuwa wakitoa huduma katika wodi hizo walisema kuwa
wanalaani kitendo cha kukamatwa na kutekwa kwa kiongozi wao wakati akiwa
anapigania haki zao.
Wakizungumza na gazeti hilo baadhi ya madaktari hao
ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa serikali inabidi itambue
kuwa wao ni watu muhimu katika taifa na kwamba kupotea kwa daktari mmoja
itawagarimu zaidi ya miaka nane kumpata mwingine.
Aidha walivitaka vyombo vyote vya usala nchini kutoa
taarifa juu ya kutekwa kwa kiongozi huyo na kupigwa kwake na kwamba pasipo
kufanya hivyo wananchi pamoja na madktari hao hawatakuwa na imani na vyombo
hivyo.
Waliendelea kusema kuwa kutokana na tukio hilo hata
yale matibabu ya dharura waliyo kuwa wakitoa kwa baadhi ya wagonjwa
hayatatolewa tena kutokana na usalama wao kuwa mashakani.
Kwa upande wao wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika
hosptalini hapo walisema kuwa mgomo huo unaendelea kuleta madhara makubwa
kufuatia idadi ya wanao poteza maisha kuendelea kuongezeka siku hadi siku.
Anna Mdapo na Halima Muhamed ni wanawake wajawazito
waliopo katika hosptali hiyo ambapo walisema kuwa serikali ni vema ikakaa na
madktari hao meza moja ili kuweza kutatua tatizo hilo kutokana na wanao
athirika zaidi ni wananchi wasio kuwa na hatia.
Hata Hivyo juhudi za kumtafuta mkurugenzi wa
Hosptali hiyo kuzungumzia tatizo hilo ziligonga mwamba baada ya kutafutwa kwa
muda mrefu na waandhi bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment