Msanii wa Kenya aliyetesa na ngoma yake ya "BANJUKA TU" miaka mitatu iliyopita aitwaye DNA baada ya kuwa nje ya game la muziki kwa muda wa miaka mitatu anzia alipotangaza kuacha muziki na kuamua kuokoka jana amewashangaza wengi alipo tangaza kuamua kurudi tena kweye game la muziki na tayari amesha achia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "MASWALI YA POLISI" sambamba na video ya nyimbo yake hiyo mpya,
Nilimuuliza maswali machache DNA, alipo ulizwa "umerudi kufanya muziki wa dunia uliokua unaufanya mwanzo?" akajibu… "ukitaka kuiita hivyo itakua hivyo lakini mi naona tofauti, sio
kama nimerudi nyuma naona kama nimesonga mbele kwa vile mtu
anavyoendelea kukomaa kwa maisha anaendelea kujua mengi na nimepata
kuona kwamba muziki wangu wa kitambo unaweza bado kutumika kwenye kazi
zangu bila kushikanisha na ule uraibu ambao nilikua nimeshikanisha nao. "
DNA amesema ameamua kurudi kwenye game ya muziki baada ya kuona mashabiki wake wamemiss ngoma za ukweli.. Hyao ni maneno yaliyotoka kinywani mwa msanii wa huyo anaekwenda kwa jina la DNA.... unajua ni nini kitafuata baada ya ngoma yake hiyo mpya?
Habari zaidi kuhusu DNA utazipata hapa hapa...
No comments:
Post a Comment