Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 29, 2012

RAY, MAINDA WABAMBWA LAIVU...!

 
 
Na Shakoor Jongo
MASTAA wawili katika tasnia ya filamu Bongo ambao wanatajwatajwa kuwa ni wapenzi wa siku nyingi, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Ruth Suka ‘Mainda’ juzikati walinaswa ‘live’ katika mapozi yaliyoacha vingi viulizo.
Wawili hao walibambwa ndani ya Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempinski, Posta jijini Dar, usiku wa Juni 23, mwaka huu kulikokuwa na uzinduzi wa Filamu ya Super Star ya Wema Sepetu.
Wakiwa ukumbini hapo, Ray alionekana akimshika mkono Mainda kama mtu aliyemtaka waondoke lakini pia akaonekana akimnong’oneza jambo demu huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja walichokuwa wakiteta lakini baada ya muda, msanii Steven Mangere ‘Nyerere’ alitokea na kumkumbatia Mainda huku akitaka kuondoka naye.
Wakati Steve akifanya hivyo, Ray alionekana akimuonya kitu Mainda huku akimnyooshea kidole ambapo mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo alisikika akisema: “Mh! Sijui huyu Ray na Mainda bado ni wapenzi au wameshabwagana, maana mapenzi ya mastaa yamekuwa ni kizungumkuti siku hizi.”
Ijumaa lilizungumza na Mainda kutaka kujua kama bado anatoka na msanii huyo lakini alijibu kwa kifupi: “No Comment.”

No comments:

Post a Comment