Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 29, 2012

RECHO AZABWA VIBAO NA MPENZI WAKE...!


Rachel Mrisho ‘Recho’.

Na Imelda Mtema
KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu Bongo, Rachel Mrisho ‘Recho’ hivi karibuni alijikuta akizabwa vibao na mpenzi wake aitwaye Saguda baada ya kutokea hali ya kuzinguana.
Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu kwenye Hoteli ya Hayyat Regency (zamani Kilamanjaro Kempinski Hotel) mishale ya saa 7 usiku, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Awali, Saguda na Recho walionekana wakizozana wakati wakitoka kwenye hoteli hiyo kulikokuwa na uzinduzi wa filamu ya Wema ya Super Star.
Mara Saguda akamnasa vibao Recho, kitendo kilichomfanya demu huyo aangue kilio na kuondoka eneo hilo akiwa amenywea.
Jitihada za paparazi wetu kuongea na mmoja kati ya wawili hao hazikuzaa matunda ila rafiki wa Recho aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya Ijumaa kuwa, chanzo cha Saguda kutoa kipigo hicho ni baada ya kuhisi anasalitiwa.

No comments:

Post a Comment