Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 29, 2012

JACK WA CHUZ ADAIWA KUTAMBA NA MAGARI YA KUKODI...!

 
Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’.

Na George Kayala
MKALI wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ amechafuka baada ya kudaiwa kukodi magari ya watu na kudai ni yake.
Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa msanii huyo zilisema kuwa, ili aonekane naye ni matawi ya juu, Jack hukodi magari kila siku baada ya kuona marafiki zake kadhaa wanatanua na mikoko ya kifahari.
“Namshangaa rafiki yangu Jack, amekuwa na kawaida ya kukodi magari na kuzunguka nayo katika ‘mishemishe’ zake na huwaambia watu kuwa ni yake,” alisema swahiba huyo wa Jack aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimpigia simu staa huyo na kumsomea tuhuma zake ambapo alisema:
“Jamani, kwani mimi sina uwezo wa kununua gari mpaka nitumie magari ya kukodi. Sijui watu wananionaje mimi, nakuambia mwandishi huwa sina kawaida ya kubadili magari bali natumia la kwangu.”

No comments:

Post a Comment