Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 16, 2012

SAKATA LA DOGO JANJA NA MADEE LAZIDI CHUKUA KASI


 SAKATA LA DOGO JANJA NA MADEE LAZIDI CHUKUA KASI


Siku moja baada ya dogo Janja kufukuzwa Tip Top Connection,ukweli halisi wa sakata hilo umewekwa wazi na yeye mwenyewe baada ya kufunguka kwa MillardAyo wa Clouds Fm
Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba dogo Janja alianza kulewa sifa na kuwa mtoro wa shule huku akijihusisha na starehe za hapa na pale mjini.

Kwa mujibu wa interview (ya pili kufanyiwa baada ya amplifaya cha jana)kwa simu saa moja asubuhi june 14 akiwa stand kurejea nyumbani ,amesema uonevu plus dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi mjini Dar es salaam
Anasema tangu aje Dar hajawahi kusaidiwa chochote na Madee,huku akidai kuwa huku huduma zote kama kula,ada ,kulala na issues zingine akisaidiwa na mtu baki.
Alizidi kufunguka dogo Janja kwa kusema,kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu huku ngoma zake zikisikika kila kona nchini Tanzania,huku show zake zikienda kwa dau si chini ya milioni za ki Tz ,kilichokuwa kinamsikitisha ni kulipwa kiasi cha laki mbili 200000 hivyo kumfanya aishi kwa taabu huku akiwa na uwezo mkubwa tuu!
Nilikua navumilia tuu,kwa sababu kila nilipokua nadai hela za show Madee alikua mkali sana,hivyo ilinilazimu kukaa kimya,anasema ilifikia kipindi alikua akifanya show za ukumbini huku akiambulia elfu 50 au mara nyingine asipokee kabisa posho!
Tamaa ilimwingia Madee kiasi cha kuninyang'anya kadi yangu ya bank na kuanza kuchukua pesa kwenye account huku nikishindwa kuelewa password aliipata wapi!kuna wakati nilitaka kumtumia MAMA hela lakini Madee alinikataza akidai kuwa watadhani nina hela 
mpaka akifanyiwa interview asubuhi alisema kadi yake ya bank mpaka sasa kadi yake imebakiwa na sh elfu 25 tuu,juzi Madee alimpigia simu akimtaarifu kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa sh laki moja "hivi bro mimi kweli ni mtu wa kulipwa laki moja''? hata hivyo ilibidi aende ili kuepusha shari.
Anasema baada ya show yeye na back up artist wake walirudishwa saa 7 usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kuwahi shule kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia,anasema inamuuma sana baada ya kuona mziki haujamsaidia chochote mpaka huku Madee akimtumia kujinufaisha na kufikia hatua ya kumalizia kujenga nyumba yake,aliendelea kufunguka zaidi na kusema "ni kama vile Madee alinipanda ili anivune" hiyo juzi wakati Tip Top wakitangaza kumfukuza yeye alikua kwa Tunda Man wakipiga story,ndipo Madee alipomuita na kuanza kumpiga!
Jamaa alinipiga na kisha kuchukua simu yangu na kuondoka nayo,huku akijitumia msg mbaya na kujijibu yeye mwenyewe akidai kuwa nilikua nataka kumroga na mambo mengine wa kadhaa,hizo msg zipo na nilimuonesha mpaka MillardAyo wa clouds fm,aliskitika sana!

Anasema simu yake alipewa jana baada ya kumwambia Madee kuwa anataka kurudi kwao ndio alipoanza kutoa maneno ya vitisho kuwa watahakikisha wananibania na sitoki tena kimziki.Pia anadai Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze asifanye interview na media,walijua wakinipa nafasi nitawaumbua sana!

No comments:

Post a Comment