Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 16, 2012

WE SI UNAPENDA HIP HOP??


 WE SI UNAPENDA HIP HOP??

VAA HEADPHONE ZAKO HALAFU BONYEZA PLAY HAPO CHINI KUSKILIZA ALBUM NZIMA YA SOLO THANG!!

 




Haya nataka nikupeleke SAFARI ya huyu bwana MSAFIRI anaejulikana na nyie kama SOLO THANG na santuri yake mpya ambayo inatafsirika kama "MIMI ni MSAFIRI ujazo wa kwanza" (I AM TRAVELLAH vol 1) kwa jina lengine maarufu kama "UWEZO MIA MIA" 

Safari hii Ambayo haihitaji tiketi  bali uwe na HEADPHONE ina Vituo (nyimbo) kumi na NNE, ndani yake kuna huduma za viburudisho inayoitwa PUNCHLINES katika kukazia KIU yako na pia ni dawa tosha ya maskio yako ambayo yanaumwa ugonjwa unaosababishwa na MEDIA kwa kulazimishwa kusikiliza Usivyovitaka huku vikipakwa ladha ya BANZOKA ama BIG G ambayo utamu wake daima haudumu na una unaukinai haraka! 

Kwanza nakukaribisha kwa kusema "WELCOME" na kujitambulisha kuwa mimi ndio "TRAVELLAH" na ndio rubani wenu wa leo katika usafiri huu tunaoutumia leo ambaoni ndege kubwa zaidi duniani ya "AIRBUSS" , sio gari wala meli wala treni,kwa vile daima tunaelekea juu angani! Sina haja ya kukumbusha kuwa mimi ni "MTOTO WA DOWNTOWN" toka kitambo,nimezaliwa Dar nimekulia Dar,na kwetu ni Dar!!

Sina makuu wa kuringa kwa ajili ya umaarufu aa kujulikana sababu najua na nathamini,mimi na wewe na yule "WE ARE FAMILY" Sina noma mi na "PARTY NA MASELA" huku nikiwatambulisha wangu "SOULMATE",sababu nishagundua hapa duniani tunapita na maisha ni "KARATA TATU" ,kuna Kisu (pesa) ,Kopa (Mapenzi) na Shupa (Jembe=utafutaji)na mwisho ya yote haya ni MAVI! Kwa kifupi ni kwamba Ili nipate PESA(Kisu) na KOPA(mapenzi) nahitaji kuwa SHUPA (jembe) kwa maana ya kujituma,na hapo ntaweza kula kunywa na mwisho wa yote haya ni karata ambayo haina maana sana kimaisha MAVI! 

Najua fika ukijituma kuna "REAL POSSIBILITIES" ya kujikwamua kimaisha na kukuepusha kukaa mtaani ukiomba "SAIDIA BABA" na kujihalalisha kuwa mmoja kati ya memba wa familia ya MATONYA! Usipende na kuzugwa na unayayoyaona kwenye maisha ya wenzako kaa ukijua kuna "VIINI MACHO" hivyo kubali maisha yako na uyaishi sio unabaki kuwa mtazamaji tu!

 Hii ndio Bongo bwana ina misala na skendo kibao kama utaifananisha na demu basi unaweza iita "MISS TANZANIA" tangu alipokuwa mwali enzi za ukoloni, bwana mchonga (NYERERE)akakata utepe,bwana Mwinyi akatoa RUKHSA na bwana BEN hakutoka KAPA ma mwisho wakamuachia (HANDSOME BOY) bwana JAKAYA, kuna mengi sana hapa ambayo kichwa cha "mbana NOSE" hakiwezi kuyabuni (najimegea)! Kwa Ubunifu huo hapo juu ni dhahiri nimeonyesha nina "UWEZO MIA MIA" na "SIDHANI" kama kuna atakaeweza kubishana na hilo! 
Album hii iliyoshiba kwa sasa nipatikana kwenye maduka ya kwenye mtandao duniani kote(Itunes,Tesco,emusic,nk) tu kwa anapenda kupata dili ya kuisambaza Cds mitaa ya bongo na East Africa kwa ujumla awasiliane na
SUKA kwa kupiga namba hii +255715222911
Ahsanteni 
MSAFIRI KONDO.

No comments:

Post a Comment