Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, July 16, 2012

GARI YA MATUNDA YAPATA AJALI...!

                                    HILI NDILO FUSO LA MATUNDA LILILOANGUKA





Gari aina ya Fuso yenye namba za usajii T 473 BVQ mali ya Michael  Mkazi wa Arusha. Gari hiyo imepata ajali eneo la kambi ya Mkaa wilaya ya Arumeru, Muda wa saa 10 alfajiri leo Tarehe 16/07/2012 ambapo gari hiyo ilikua na watu watatu ambao ni Dereva wa Gari hiyo aina ya Fusa aitwaye Edwin kondakta wa gari hiyo na Mfanyabiashara wa Matunda aliyekodi Gari hiyo kwa ajili ya kubebea Matunda kutoka Tanga mpaka Arusha ambaye hakuweza kujulikana Jina.


                          HILI NDILO FUSO LILILOLETWA KUFAULISHA MZIGO

Chanzo cha ajali hiyo kinasemekana ni kutokana na kukatika kwa Tairoad hand ambayo  ilisababisha gari hiyo kuacha njia na kuingia kwenye mtaro ambapo dereva alishindwa kuizuia na kujikuta tayari Gari imelala ubavu wa kulia. Watu wote Watatu wliokua kwenye Gari hiyo ni wazima na wanaendelea vizuri. Mmiliki wa Gari hiyo alituma gari nyingine aina ya Fuso yenye namba za usajili T122 ALR kwa ajili ya kufaulisha Matunda hayo aina ya Machenza na Machungwa.

No comments:

Post a Comment