Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 15, 2012

EPUKA MAFUTA YA BEI CHEE...!

DUMU LENYE MAFUTA FEKI



Utapeli mkubwa umeibuka ndani ya Mji wa Moshi
Watu wanaojifanya ni wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya 5 Group inayojenga Jengo la NSSF Moshi wanawatapeli Madereva wa Daladala kwa ataili ya aina yake.
Watu hao huenda kwa wapiga debe na kuwaambia wana Diesel na wanauza kwa lita Tano shilingi elfu nane na Mafuta hayo yanatolewa usiku katika Eneo la ujenzi (Yanaibiwa) na wawatafutie wateja baada ya wapiga debe kutafuta wateja huwaagiza wakutane usiku karibu na eneo la jengo linapojengwa huwapa mafuta katika madumu ya maji kisha huwaambia waondoke haraka wasikamatwe

Baada ya kufika mbele hugundua yale si mafuta bali ni maji yaliyochanganywa na Mafuta kidogo.


                                               HUYU NI MTUHUMIWA WA KWANZA

Usiku wa jana Dereva wa daladala ya  Majengo kwamtei aliuziwa lita Miamoja kwa shilingi laki mbili na ishirini na tano na baasa ya kugundua alirudi eneo walipofanyia biashara akakuta jengo linalindwa na mchina na huyo waliyefanya naye biashara hajulikani

Baada ya kumkosa muhusika ilibidi wawatafute wale wapiga debe lakini baada ya kuwapata hawakuweza kuwajua wahusika sababu walikutana nao kituo cha daladala wakawapa kazi kwa makubaliano ya malipo ya shilingi elfu 10 kila mmoja ila cha kushangaza wao wenyewe wamepewa pesa za bandia kama malipo yao

Wakati tukio la kuwahoji waliokamatwa Alitokea dereva wa daladala ya pasua akasema amepigiwa simu na mtu huyo na amemwambia anauza maguta ya dili wakakubaliana wakutane leo usiku ili wafanye biashara



    MTUHUMIWA NAMBA MBILI ALIKUTWA AMELALA JUU YA MTI ULIO MAKABURINI
INASEMEKANA ANAISHI KWENYE MTI HUU

No comments:

Post a Comment