Pichani Juu na Chini ni Wanafamilia
wa Jay Dee wakipakia mizigo tayari kuelekea
kituo cha kulelea watoto
yatima cha Maunga Centre kwa ajili ya kukabidhi msaada.
Kiongozi wa msafara LadyJay Dee akielekea kupanda usafiri maalum ulioandaliwa.
Wanafamilia ndani ya basi kuelekea Maunga Cente kituo cha watoto
yatima kwa shughuli nzima ya kukabidhi msaada.
Wanafamilia Ester Ulaya Cathbert na
Maggie wakifanya shopping katika
maduka ya Kinondoni njiani kuelekea
kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.
Judith G. Habash a.k.a Komando Binti
Machozi Lady Jay Dee akiwasili na Familia yake katika Kituo cha kulelea
watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo maeneo ya Kinondoni
Hananasifu.
Vijana wa Familia ya Jay Dee
wakishusha msosi ulioandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya watoto yatima
wa Kituo cha Maunga Centre.
Baadhi ya zawadi zilizopekwa na Jay Dee Family katika kituo cha kuelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mwanafamilia wa Jaydee Wise Monica Kaaya akionyesha Upendo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi. Zainabu Bakari akionyesha chumba wanacholala watoto wa kiume katika kituo hicho.
Hapa ni mahali wanapotundikia neti.
Mtoto Khadija Mussa akisoma Risala
kwa mgeni rasmi Komando Lady Jay Dee na Familia yake (hawapo pichani)
ambapo amezungumzia changamoto ya mahali wanapoishi haparidhishi na
kuwataka wadau kujitokeza kuwasaidia kuboresha eneo lao ikiwemo Choo,
Sehemu ya kulala pamoja na ada za twisheni kwa watoto hao.
Wanafamilia wakisikiliza risala ya Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo pichani).
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady Jay Dee akikabidhi msaada
uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele, Maharage, Mafuta ya Kupikia,
Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na vingine vingi. Anayepokea
msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi. Zainabu Bakari (kushoto) pamoja
na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Khadija Mussa.
Jay Dee Family inawakaribisha wadau
wote watakaoguswa kutoa mchango chcochote walichonacho kupitia Jay Dee
Family. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto) akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay Dee.
Pichani Juu na Chini Wanafamilia wa
Lady Jay Dee wakipakua chakula kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili
ya kula pamoja na watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi
Zainabu Bakari ambapo amezungumzia changamoto zinazowakabili ni sehemu
ya kuishi wahudumu wa kituo hicho, mishahara ya kuwalipa wahudumu na
makazi ya wahudumu wa kituo hicho. Bi.
Zuhuru Bakari alisema kituo hicho kinalea watoto 30 ambapo watoto 20
wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi waliowachagua wao kutokana
na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya watoto 50.
Mwanafamilia Ester Ulaya akizungumza
kwa niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema watakuwa bega kwa bega na
kituo hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili wa kusaidia kituo hicho.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Zainul Mzige wa MO BLOG alijumuika na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Wanafamilia wa Jay Dee katika picha
ya pamoja baada ya kuhitimisha zoezi zima la kutoa msaada kwa kituo cha
watoto yatima cha Maunga Centre.
No comments:
Post a Comment