Mkali wa soka kutoka Brazil
ambae ni mwezi umepita toka aondoke kwenye club ya Flamengo aliyokua
anaichezea kutokana na kushindwa kumlipa mishahara yake, amepatwa na
tatizo jingine kwenye moja kati ya madili yake.
Kampuni ya vinywaji ya
Coca-cola imeukatisha mkataba mnene na mchezaji Ronaldinho baada ya
mchezaji huyo kuonekana akiwa na vinywaji vya Pepsi pembeni wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na club yake mpya ya
Atletico Mineiro.
Mkataba wake na Coca-cola ambao
hauna hata mwaka toka usainiwe, ulitakiwa kwenda mpaka 2014 ambapo
malipo yake kwa mwaka ni dola za kimarekani zaidi ya laki saba.
Pepsi ni wadhamini wa club yake
mpya ya Mineiro na kuwepo kwa vinywaji hivyo kwenye mkutano huo na
waandishi wa habari sio chaguo au uamuzi wa Ronaldinho, ni maamuzi ya
club kwa sababu ndio yenye mkataba na Pepsi na sio Dinho.
No comments:
Post a Comment