Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 12, 2012

MTORI WAWASAFIRISHA ASLAM NA MYLENE KUTOKA KANADA MPAKA BONGO....!

Aslam akiwa na mwanaye Samira

Jengo la Saint Mary hospital ndio Mylene mke wa Aslam alipo jifungulia.

Samira Aslam

 KUTOKANA NA MAONI YA WASOMAJI KUTAKA KUPATA STORY MOJA KUTOKA KITAA LEO NIMEONA NIANZIE CANADA.. Kuna mshkaji mmoja anitwa Aslam Ramadhani Topiwala, mshkaji ni mwenyeji wa Arusha ila kwa sasa yupo Canada sehemu moja inaitwa  Montreal, nilifanikiwa kupiganae story kupitia skye na haya ndio aliyonieleza.

 King Jofa: Mambo vipi kaka?
Aslam: Mzuka kaka Mimi Aslam Ramadhani Topiwala, Dem wangu Anaitwa Mylene Dimitri,  nilikutana nae Arusha anafanya kazi UN( defence Lawyer kwenye tribunal of Rwanda genecide)
NIlikuja Montreal Canada kwa Ajili ya maandalizi ya Kuzaliwa kwa mtoto wetu Samira Aslam Topiwala.
  King Jofa:Hongera sana kaka, vipi lakini hali ya mwenzi wako kwa sasa?
Aslam: Wife tayari ameshajifungua tokea tarehe 4 mweziwa saba mwaka 2012 wife alikaa siku mbili tu akaruhusiwa kurudi nyumbani..
King Jofa: Kuna tofauti gani ulizoziona za huduma ya afya za Tanzania na huko Canada?
Aslam: huku kila raia ana health insurance Tofauti kubwa nimeiona Hospitali ambako madaktari wako Fasta sana kama mtoto akizaliwa na shida . kulikuwa na Madaktari Wanne wakati anajifungua na Manesi wawili na Mtaalam mmoja wa ajili ya kutatua tatizo la mtoto alipokuwa anapumua kwa shida. Mtoto sasa yuko safi na Tuko Nae nyumbani.

King Jofa: Shukrani sana brother... Unategemea kurudi lini nyumbani (Tanzania)
Aslam: Nategemea Kurudi Tanzania - Arusha kabla ya Tarehe 20 Mwezi huu wa saba  Kuendelea Na Ujenzi wa nyumba yangu Pale ilboru ambako ntaishi na wife na Mtoto wangu Inshaallah itakapo malizika mwisho wa mwaka huu.

King Jofa: Wanawake wa kiafrica/Tanzania wameshazoa wanapojifungua huwa wanakunywa uji na mtori kwa wingi, vipi kwa wife wako ambaye si mtanzania je ataweza kunywa mtori na uji?
Aslam: Kwa uopande wa msosi nasubiri kwa hamu tufike Home ili Mama Ampikie Mylene Mtori wa Uhakika Kujenga afya.
 


No comments:

Post a Comment