Panone and company Ltd. and Ngiloi Ulomi Enterprises yenye vituo vingi vya Mafuta na Wasafirishaji wa Mafuta Afrika
Mashariki Na kati Walifanya promotion ya wiki nzima lengo likiwa ni kuendelea kuwapa wateja wake huduma iliyo bora na kwa wakati sahihi. Kwa wiki nzima waliweka utaratbu wa kila mteja atakayefika kwenye kituo chao cha mafuta kilichopo mkoani kilimanjaro anapatiwa huduma safi na pia anapewa tiketi ambayo inamuwezesha kushiriki katika shindano la kupata lita 100 za mafuta, na kama hiyo haitoshi pia walitoa tiketi kwa wateja wao walio nunua bidhaa mbalimbali katika supermarket zao.
Nilifanikiwa kuongea na Gido Marandu ambaye ni Managing Director wa Panone and Company Ltd. na kunijuza kuwa "hii ilikuwa ni Promosheni ya Wiki iliyoanza Tarehe 09/07/2012
na kufikia kilele Jumamosi ya Tarehe 15/07/2012 imeanzia Moshi na baadae itaendelea kwenye mikoa mingine kama Arusha, Manyara, Tanga na kwingineko kote nchi nzima, lengo likiwa ni kuendelea kuwanufaisha wateja wake ili waendelee kwenda kujipatia huduma katika vituo vyao vya maafuta vilivyopo nchi nzima, na pia nawashukuru sana wateja wetu kwa kwa kuipokea promotion hii vizuri na kwa ushirikiano mkubwa"
Pia walifanikiwa kupata washindi kumi na moja ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Bw. Saimon Urio mwenye gari aina ya corolla yenye namba za usajili T208 AQT aliye jishindia lita hamsini za mafuta (petrol). Mshindi wa pili alikuwa ni Bi. Marium, aliye jishindia lita 20 za mafuta ya kupikia, Na Mshindi wa tatu alikuwa ni Bw, Mmoja ambaye hakuwa ameandika namba za simu wala jina ila uongozi wa Panone una namba za gari yake na utamtafuta ili aweze kwenda kujipatia zawadi yake.
Managing Director wa Panone Gido Marandu alielezea kuhusu uchakachuaji wa mafuta na kusema kuwa yeye anawatupia lawama madereva wenye tamaa ambao ndio hufanya mchezo huu mchafu wa kuchakachua mafuta. Lakini aliendelea kueleza kuwa kampuni ya Panone wameweza kudhibiti hali hiyo ya uchakachuaji wa mafuta kwa kuwa kila dereva anakuwa na msimamizi wa kumlinda ili asiweze kuchakachua mafuta wakati wa kuyasafirisha kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine. Gido Marandu aliendelea kutoa ushauri kwa wafanya biashara wote kuwa siri ya kufanikiwa katika biashara ni kujitahidi kutoa huduma ya uhakika na sio longolongo.
Gido Marandu Managing director wa Panone and company Ltd. and Ngiloi Ulomi Enterprises
Casim Mwinyi (BaBi) akiwa na Gido Marandu wakati wakiwapigia simu washindi wa promotion wiki iliyofanyipa eneo la sheli ya Ngiloi Ulomi Enterprises mjini Moshi.
*KARIBUNI SANA PANONE AND COMPANY LTD na NGILOI ULOMI ENTERPRISES*
No comments:
Post a Comment