Mahakama kuu kitengo cha kazi imetoa hukumu juu ya shitaka lililokuwa mahakamani hapo juu ya walimu kugoma wakidai nyongeza ya mishahara na baadhi ya malimbikizo ya mishahara ambayo wanaidai serikali. Mashitaka hayo yamegongwa mwamba baada ya hakimu kuamuru waalimu wasitishe mgomo kwa kuwa taratibu walizo zitumiamgomo kuanzisha mgomo huo ni batili.
Mahakama hiyo ya kazi imemtaka Kiongozi wa wa waalimu aliyetangaza mgomo huo kusitisha mara moja na walimu warejee mashuleni kuendelea na kazi kama kawaida. Pia mahakama hiyo imeiamuru CWT kuwalipa fidia wanafunzi wote walio athirika na mgomo huo.
Swali kubwa ninalojiuliza ni je mahakama imetenda haki?
Na kama imetenda haki Waalimu wameridhika na hiyo hali?
Na mahakama inafahamu umuhimu wa mwalimu katika kulijenga taifa?
Waalimu wanarudi mashuleni wakiwa na hali gani?
Je utendaji wa kazi utakuwaje huko mashuleni baada ya maamuzi ya mahakama?
Baada ya maamuzi hayo ya mahakama nilibahatika kuongea na mwalimu wa shule ya secondali iliyopo Moshi japo hakutaka jina lake litajwe. yeye alinieleza haya "Kweli walimu hatujatendewa haki na maamuzi hayo ya mahakama yamefanyika bila kufikiria madhara ya baadae, Je tukirudi mashuleni tukiwafundisha wanafunzi kuwa 7+7=77 au tukiwaambia binadamu wa kwanza alikuwa Nyerere... unadhani hasara itakuwa ya nani?" mwisho wa kunukuu..
Hiki ndicho kitakachoendelea endaponwalimu watalazimishwa kurudi mashuleni pasipokuwa na maelewano kati yao na serikali
No comments:
Post a Comment