Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo
la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha
Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe
1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama
kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na
athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa
Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani
Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji hicho cha
Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa
wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na
Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na
ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha
Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa
ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha
kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na
ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Kikwete akiwa na Viongozi wengine Meza kuu.
Rais Kikwete akielekea kwenye Jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hafafika na kuigawa
kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha
kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake
uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila
mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na
Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000
kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia kwake ni Mbunge
wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza kuwakumbuka
wananchi wa Wilaya ya Mbonduli.
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa baada ya kufanyika kwa mpango wa
kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa
Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana
na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng'ombe kwa wananchi wa wilaya tatu
za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo
800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiwa katika Mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher
Ole Sendeka.
Mh. Lowassa na Mh. Lukuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli.
Burudani kutoka kwa Vijana wa JKT.
No comments:
Post a Comment