Dar es Salaam, TANZANIA– shirika la ndege la Qatar, ambalo linamilikiwa na serikali
ya nchi ya Qatar imeanzisha rasmi njia rahisi na ya haraka ya kutoa
huduma zake kwa wateja wake ambapo tiketi za safari za anga zinazotolewa
na shirika hilo zitatolewa pia kwa njia ya mtandao wa kulipia kupitia mtandao wake wa usajili wa safari na kupitia kwenye tovuti ya www.qatarairways.com/tz.
Muundo huu mpya utawapa nafasi wateja wote kubook tiketi zao kwa njia ya mtandao na kulipia baadaye kuzichukua katika ofisi za Qatar. Malipo lazima yawe yamekamilika katika masaa 48 na hamna
malipo yoyote ya ziada kwa wanaofanya malipo haya kupitia
mtandao.Malipo yakishafanyika, wanaweza wakafanya ‘online check in’ na
wanaweza pia kuchagua viti wanavyovipendelea na kichangua pia mlo ambao
wangetaka.
Wale wanotumia kadi za malipo ya baadaye yaani ‘credit cards’ wanaweza
wakamaliza kubook, kununua na kufanya kila kitu hapo hapo kwenye
mtandao.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hili, Bw. Akbar Al Baker alisema kwamba mfumo huu mpya wa malipo inawapa wateja njia mbadala ya kununua tiketi zao
“Wateja wetu wanaweza sasa kununua tiketi zao wakiwa mahali popote na huduma hiiinatolewa masaa
ishirini na nne siku saba kwa wiki na kwa hapo hapo kuweza kujiunga na
ofa zinazokuwepo mara kwa mara. Ni mfumo rahisi tu kutumia na pia
inakupa wewe mteja wetu uwezo wa kuchagua njia tofauti tofauti za
kupanga safari zako.”
“Shirika la ndege la Qatar
limejikita kuendeleza na kuboresha huduma zake ili kurahisisha na
kufanya usafiri wa anga wa kwa wateja wetu kuwa mzuri na rahisi.
“alisema
Kampuni hii iliyokuwa na makao makuu yake Doha nchini Airways juzi ilizindua mtandao wake ambao rahisi kutumia na pia ambao umetengenezwa ukizingatia mahitaji ya wateja wote. Mtandao huu unakuwezesha kupata kuona kurasa nyingi na kufanya booking za safari zako kwa urahisi zaidi.
No comments:
Post a Comment