Wahamiaji haramu 27 kutoka nchini Somalia wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Canter kupata ajali katika barabara ya Moshi-Himo eneo la daraja la Kilimapofo Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boazi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi, huku mmoja kati ya majeruhi hao amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
Amesema gari hilo lilikuwa limebeba jumla ya wahamiaji haramu 39 na kati ya hao 27 ndio walioumia kutokana na ajali hiyo ambapo wahamiaji wengine ambao hawakuumia wanaendelea kushikiliwa na polisi katika kituo cha polisi Moshi mjini.
Kamanda ameongeza kuwa wahamiaji hao bado haijafahamika mara moja walikuwa wakielekea wapi na mahojiano kati yao na polisi bado ni magumu kwa kuwa wahamiaji hao hawafahamu lugha ya Kiswahili wala kiingereza.
Amesema awali walipata taarifa hizo kutoka kwa wananchi ndipo jeshi hilo likaweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.
Katika hatua nyingine kamanda Boaz amesema pia jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata wahamiaji haramu wengine watano leo asubuhi wakiwa wamejificha mashambani wakisubiri usafiri.

No comments:
Post a Comment