TAARIFA HII IMETOKA MOJA KWA MOJA KWENYE MIKONO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA VIJANA (BAVICHA)
Ndugu Wanajukwaa,
Taarifa za kuvuliwa uanachama kwa Juliana Shonza (Makamu Mwenyekiti BAVICHA), Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni za kweli!
Hatua hii ilifikiwa jana na kikao cha kamati tendaji ya BAVICHA iliyokutana pale Ukumbi wa Mbezi Garden majira ya Saa sita na nusu Mchana.
Kikao hiki kimsingi hakikuweka wazi ajenda za kwenda kujadili uanchama wa wahusika hapo juu (Pitia taarifa ya Tumaini Makene hapa JF kuhusu kikao hicho) licha ya wahusika hao hapo juu kualikwa kuhudhuria kikao hicho.
Wajumbe walioalikwa kwa ajili ya kikao hiki ni kama wafuatao: (Hawa wahusika si wajumbe wa kikao cha kamati tendaji BAVICHA)
1. Ben Saanane
2. Chacha Hatari
3. Habib Mchange
4. Mtela Mwampamba
5. Gwakisa Burton Mwakasendo.
Hao wajumbe hapo juu walihojiwa na kamati tendaji kila mmoja kwa nafasi yake na mashitaka yake mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la vijana Ndugu John Heche na katibu Deo Munishi.
Naomba kuyaweka mahojiano kama ifuatavyo, (mahojiano yalianza kufanyika saa tatu na nusu usiku).
Ben sanaane alihojiwa kwanini ametoa shutuma kali mitandaoni kwa viongozi wake wa juu (Zitto)?
Majibu ya msingi ya Ben Saanane yalikuwa ni kwamba aliamua kufanya vile kwasabu ya kukilinda chama na viongozi wake wasihafuliwe mitandaoni na vijana aliowataja ni 'Masalia'.
Swali likaja; yeye haoni kama alikuwa anamchafua Zitto ambaye ni kiongozi wa chama? Jibu lake lilikuwa ni kuomba radhi amekosea.
Mtela mwampamba alihojiwa kwa kuulizwa mashitaka mawili. Moja ni kwanini anampinga Dr. Slaa kuwa anamiliki kadi ya CCM na pili kwanini alimkashifu Dr. Slaa hapa JF kwa kutumia 'Verified Account'Majibu ya Mwampamba ni kama ifuatavyo:Kwanza alianza kwa kuomba kubadilishiwa mwenyekiti wa kikao kwasababu hana imani naye. Kwanini hana imani naye? Ni kwa sababu wana 'conflict of interest' kwenye siasa (kuanzia kwenye uchaguzi wa BAVICHA) hawaelewani hivyo anaamini haki haitatendeka endapo Heche atasimamia mahojiano yale.
Mjumbe mmoja (mwenyekiti Arusha) akanyoosha mkono kwa kusema asiwasumbue wapo kazini. Mwampamba akajibu, hata mbunge wa Arusha Godbles Lema aliomba kubadilishiwa jaji kwenye kesi yake kwasababu alikuwa hana imani naye. Mwampamba akaongeza kwa kusema Ibara ya 18 na 19 ya katiba mama ya nchi inampa uhuru wa kuchagua nani wakusikiliza maoni yake na haki ikatendeka.
Mjumbe mwingineakasimama akasema kuwa yeye ameacha kata yake na kuja kusikiliza, Mwampamba unatusumbua. Mwampamba akamjibu mimi nimeacha wanachi 32,000 kule Mbozi jimboni (alikogombea ubunge mwaka 2010) wanaonitegemea nimekuja hapa, wewe unataka kusema ndio unajua sana kazi?
Kilichotokea: Bwan John Heche akagadhabika na kuamuru mabaunsa sita (6) wakiongozwa na Baunsa wa Mbowe anayejulikana kwa jina la 'Swai' wamtoe nje. Mwampamba alitolewa nje kwa nguvu, akatoka!HABIB MCHANGE:Yeye alikuwa na shitaka la kuwakashifu viongozi mitandaoni. Habib Mchange akahoji kwa mwenyekiti wa kikao. Kwanza alihoji uhalali wa kikao, kwasababu kile kikao kikatiba hakipo kwasababu hakuna makatibu wa baraza la vijana ni kikao cha wenyeviti tu? Pia, akaomba aelezwe ameitwa kama nani kwenye kikao kile? Pia akaomba apewe mashitaka yake yenye uthibitisho wa yeye kuhusika na hayo wanayo yasema.
Mwenyekiti kwa hasira akaamuru mabaunsa wamtoe Mchange nje! Mchange kwa ustaarabu akatoka nje.Gwakisa Burton:Yeye alikuwa na mashitaka mawili la kumpinga Dr. Slaa kuwa na kadi mbili ya CHADEMA na CCM pamoja na kumpinga Sugu Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA).
Bila kuchelea Gwakisa akakili kweli alimpinga Dr. Slaa kwa kumiliki kadi mbili, Pia alikili alimpinga Sugu kwasababu wanatofautiana kimawazo (ikumbukwe Gwakisa alitolewa kwenye kura za maoni jimbo la Mbeya Mjini ili Sugu apitishwe kuwa mgombea). Alichokifanya mwenyekiti John Heche palepale akaamuru kumsamehe Gwakisa na kupewa onyo kali la kutorudia tena kuwapinga viongozi wake.
Ndugu wana JF,
Kikao kilimalizika mnano saa 5 na dakika 46 usiku. Maazimio ya kikao kile ni kuwavua uanachama wahusika watatu hapo juu.
UTATA ULIPOJITOKEZA:
Kimsingi katiba hairuhusu kabisa na haiwapi mamlaka BAVICHA kufukuza uanachama mtu yeyote. Kwenye katiba hakuna sehemu kamati tendaji inapewa nafasi ya kuhoji na kufukuza wanchama ndani ya chama.
Pia, Juliana Shonza atavuliwajwe uongozi na kamati tendaji wakati katiba inaeleza wazi kuwa mkutano mkuu utaitishwa lilikumvua uongozi kwa sababu yeye alichaguliwa na mkutano mkuu?
HATUA ALIYOICHUKUA FREEMAN MBOWE:
Nimetoka makao makuu ya CHADEMA muda huu pale Kinondoni, wameandaa toka asubuhi eneo, ambapo palitakiwa pafanyike Press Conference na vyombo vya habari kuhusu maazimio ya jana kwenye kikao. Freeman Mbowe amezuia hatua hiyo ya kutangaza maazimio hayo kwa sababu BAVICHA hawana mamlaka ya kumuwajibisha mwanachama yeyote, Kinachotakiwa BAVICHA kukifanya ni kupeleka mapendekezo yao kamati kuu ya CHADEMA taifa ndiko maamuzi yote yatafanyika.
Kwa maana hiyo John Heche na Mbowe wapo kwenye msuguano mkali,Kutokana na kwamba hili swala likifika kamati kuu litakwend akinyume na wanavyotaka.wajumbe wengi wa kamati kuu wanaendesha mamuzi yao kiutuuzima,bila hisia na kikatiba. Pia uzito wa makosa haya haupelekei kupoteza vijana hawa wenye umuhimu mkubwa kwenye majimbo yao na kwenye chama.KUHUSU JULIANA SHONZA:Yeye hakufika kwenye kikao kile kutokana na kutokuwepo jijini Dar es Salaam na taarifa kuchelewa kumfikia. Hivyo walishindwa kufanya mahojiano naye na kumpatia mashitaka yake.
HALI NDANI YA KIKAO ILIVYOKUWA:
Wajumbe walionekana kuandaliwa ipasavyo kisaikolojia kwaajili ya kuwakabili Mwampamba na Mchange. Kwa sababu walipoingizwa kwenye ukumbi wa kikao kila mmoja alitengewa kiti chake na kukabishiwa mabaunsa 6 kwa ulinzi. Muda wote Mwampamba na Mchange walikuwa kwenye ulinzi mkali sana.
Waalikwa wengine kama Saanane na Gwakisa na hatari walikwa hawana ulinzi, wapo free.
MWISHO:
Hii ndio CHADEMA, kuna uwezekano wa wanachama wengi wakafukuzwa kwa kupigiwa simu tu bila katiba kufuatwa. Pia kufukuza wanachama ndio last solution kwa kulea vijana?
Chanzo: JAMIIFORUM/Jukwaa la siasa

No comments:
Post a Comment