Mbunge wa
Jimbo la Arusha, Godbless Lema amewataka wakazi wa Arusha, kujiandaa kwa
maandamano hadi bungeni Dodoma, kupinga kuwasilishwa muswada wa
mabadiliko ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, badala ya 2015 ufanyike 2017. Akizungumza
katika mkutano wa kampeni jana katika Kata ya Kaloleni, Lema alisema
kuna taarifa kuwa kuna mpango wa kupelekwa bungeni muswada wa mabadiliko
ya uchaguzi ujao, jambo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
“Tunajua
wabunge wa CCM wataukubali muswada kwani wanajua ukifanyika Uchaguzi
Mkuu mwaka 2015 wengi hawatashinda, lakini wajue nguvu ya umma
itashinda,” alisema Lema.
Lema ambaye
kesi yake ya kufanya vurugu Chuo cha Uhasibu Ausha, imepangwa kuanza
kusikilizwa Julai 2 baada ya upelelezi kukamilika, alisema kuna hoja
kuwa Uchaguzi Mkuu lazima ufanyike baada ya kukamilika kwa mchakato wa
Katiba Mpya au kuwapo na fedha za kutosha jambo ambalo Chadema
hawatalikubali.
“Tunajua
mwaka 2015 Chadema tunachukua nchi hivyo, hatutaki kuwaongezea muda CCM
na tukichukua nchi tu kama nikichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani
katika kipindi cha miezi sita kitaeleweka,” alisema Lema.
Alisema
ndani ya miezi sita Serikali ya Chadema,itahakikisha fedha zote
zilizofichwa Uswisi na nchi nyingine zinarudi na watuhumiwa kufikishwa
mahakamani.
Akizungumzia
uchaguzi mdogo wa Kata ya Kaloleni,Themi, Kimandolu na Elerai,Lema
alisema chama hicho kina uhakika wa ushindi kwani wagombea wake
wanakubalika na wana uwezo.
Hata hivyo,
aliwataka wakazi wa Kaloleni na kata nyingine, kujitokeza kwa wingi
kupiga kura June 16, ili mchana tayari wawe wanashangilia ushindi.
Lema alisema
wanataarifa za kugawanywa fedha mitaani, akawataka wafuasi wa Chadema
kuzichukua fedha hizo kwani ni kodi zao, lakini kura wapige kwa Chadema.
Awali
mgombea wa udiwani wa Chadema wa kata hiyo, Emanuel Kessy alitoa ahadi
kuwa akichaguliwa,atahakikisha wazee wote wanatibiwa bure, hakuna watoto
wa shule watakaorudishwa nyumbani kwa kukosa ada pia ataimarisha usafi
wa kati hiyo.
Mgombea wa
udiwani wa Kata hiyo kupitia CUF, Abbas Mkindi maarufu kama Darwesh
akizungumza katika kampeni juzi hiyo , aliwataka wakazi wa kata hiyo,
kutofanya makosa kuchagua watu wasio na uchungu na kata hiyo.
“Mimi mnanifahamu hapa, nimezaliwa hapa, tumekuwa wote hapa,na hivyo najua shida zetu naomba mnichaguwe,” alisema Mkindi.
Chanzo - Mwananchi
No comments:
Post a Comment