Muonekano wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
MOSHI Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Moshi kimeanza kutekeleza agizo la
mwenyekiti wa taifa wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete la kutoa mafunzo kwa watendaji
wake kuanzia ngazi za matawi na kata ilikutambua wajibu wao katika kuitumikia
pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika manispaa
hiyo kwa niaba ya katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi katibu
wa CCM wa Manispaa ya Moshi Aluu Segamba alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa
watendaji wa chama hicho pamoja na jumuiya zake.
Segamba ameyataja mambo yatakayofundishwa nipamoja mada mbalimbali zikiwemo uandaaji wa vikao,utawala bora, uandaaji wa mikutano ya hadhara pamoja na muongozo wa utunzaji wa fedha na mali za Chama Cha Mapinduzi.
Nao baadhi ya watendaji waliyoshiriki katika mafunzo hayo wamesema kuwa yamewajengea ujasiri mkubwa hivyo wataweza kufanya kazi zao kwa kujiamini zaidi kwakuwa wametambua nini wajibu wao katika kukitumikia chama na jamii kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment