Meneja wa Kampuni na muwakilishi wa Panone ndugu Gido Marandu akizungumza katika uwanja wa indu mandal mjini Moshi kabla ya kuanza kwa mpambano kati ya Ally Baba kutoka Moshi na Chilambo Hemed kutoka jijini Dar es salaam
Bondia Ally Baba aliyevaa kampula nyeupe na bondia Ambilikile Chunya aliyevaa kampula nyeusi.
Ally Baba kutoka Moshi na Ambilikile
chunya kutoka jijini Dar es salaam
chunya kutoka jijini Dar es salaam
Bondia Ambilikile Chunya akipewa huduma ya kwanza na kocha wake baada ya kuanguka chini kufuatia konde zito alilopigwa na Ally baba.
Bondia Ambilikile Chunya akijaribu kunyanyuka ili aweze kuendelea na mpambano lakini alishindwa kunyanyuka.
Bondia Ambilikile Chunya akimtizama mpinzani wake Ally Baba kwa hasira lakini hakuwa na lakufanya maana tayari refa alishasimamisha mpambano akiashiria ushindi kwa ally Baba.
Bondia Ally Baba akiwa amembeba mwanae mabegani wakishangilia ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Ambilikile Chunya.
Leo katika viwanja vya hindu
mandali vilivyopo Mkabala na stand kuu ya Mabasi mjini Moshi
kumemalizika Pambano kali la Ngumi kati ya ,Ally Baba kutoka Moshi na Ambilikile Chunya kutoka jijini Dar es salaam. Pambano hilo ambalo
limedhaminiwa na Kampuni ya Panone and co. ltd. Pambano hilo lililoamsha hari kubwa na msisimuko wa aina yake na kudhihirisha kuwa mchezo wa masumbwi unapendwa sana na wakazi wa mjini Moshi kwa jinsi walivyokuwa wakishangilia kwa shauku kubwa. Mpambano huo ulimalizika kwa Ally Baba kuibuka mshindi kwa kutoa mpinzani wake kwa Knock Out katika round ya nane ambayo ilikua ndio round ya mwisho ya mchezo huo.
Pambano hilo lilitanguliwa na mapambano ya awali ambapo pambano la kwanza lilikuwa kati ya bondia wadogo waliotoka Arusha ambao ni Lenox Mroso na Holfild Mroso hatimaye Lenox Mroso aliibuka mshindi. Mpambano wa pili ulikuwa kati ya Dickson Feldnand na British Filex ambapo Dickson Feldnand alishinda kwa points 39 dhidi ya points 37. Mpambano wa tatu ulikuwa kati ya Abdalah Mwakipesile na Emmanuel Filex mpambano huu uliishia round ya kwanza ambapo Emmanuel Filex alimshinda mpinzani wake kwa knock Out. Mpambano wa nne na wa mwisho kwa upande wa utangulizi ulikuwa kati ya Paskal Bruno na Godfrey Magunga ambapo mshindi alikuwa ni Paskal Bruno kwa kumshinda mpinzani wake kwa points 39 dhidi ya 37.
Akizungumza katika
ufungaji wa Pambano hilo Meneja wa Kampuni ya Panone ndugu Gido Marandu
alisema "hii ni fursa ya pekee kwa kampuni ya Panone kuhakikisha mchezo huu
unafanikiwa na katika kuhakikisha hilo kampuni ya Panone imeweza kujitoa ipasavyo
katika hilo." Aliongezea kwa kusema kuwa "huu ni mwanzo kwa kampuni ya Panone kukuza
michezo ndani ya Mkoa wa kilimanjaro na alitoa wito kwa
vijana kujikita katika michezo ili kujiepusha na Tabia hatarishi ambazo
zinaweza kuhatarisha maisha yao huku akitoa Mfano wa Timu Ya Panone Fc
ambayo inamilikiwa na Kampuni hiyo ni timu ambayo inaundwa na vijana
wenye moyo na hari ndio maana wamepata mafanikio kwa muda mfupi hivyo
vijana waige mfano huo katika michezo."
No comments:
Post a Comment