Muwakilishi wa Panone and co. ltd, Kassim Mwinyi akipeleka tisheti za watoto katika kituo cha SALAM CENTRE.
Afisa masoko wa Panone ndugu Frank
Mwaikatale akikabidhi tisheti za watoto wa kituo cha SALAMA CETRE kwa mlezi wa watoto hao Bi. Upendo.
Afisa masoko wa Panone ndugu Frank
Mwaikatale akiwakabidhi baadhi ya watoto wa kituo cha SALAMA CETRE namba za kushiriki katika mbio za Kilimanjaro marathon.
Panone and co. ltd ni kampuni ya
Usambazaji na uuzaji wa mafuta ya magari jumla na rejareja. Ikiwa
imejikita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kuhakikisha inatoa huduma
bora kwa wateja na kwa masaa ishirini na nne yaani usiku na mchana. Katika kuhakikisha jamii
inapatahuduma Muhimu katika kila kituo kuna supermarket na huduma ya
kibenki na kifedha kupitia simu ya mkononi M-Pesa inayopatikana muda
wote. Panone and co. ltd ina bakery ya kisasa ambayo kwa sasa inazalisha
mikate inayokwenda kwa jina la Panone Bread, Queen Cake, Pan Cake,
Maandazi na pia inafanya Parking ya Mchele, Korosho, Karanga vyote
vikiwa katika nembo ya Panone.
Akizungumza na Mwanahabari wetu Afisa masoko wa Panone ndugu Frank
Mwaikatale alisema Panone katika kuhakikisha inashiriki vyema na Jamii
na kuthamini michezo imeweza kudhamini timu ya riadha ya Mkoa kilimanjaro
ilikuhakikisha inashirikivyema katika mbio za kimataifa za Kilimanjaro
Marathon. Mbali na timu hiyo pia imeweza kutoa Udhamini kwa watoto
waishio katika mazingira Magumu wanaolelewa katika kituo cha SALAMA
CENTRE kilichopo Majengo Moshi. Udhamini huo ni katika kuhakikisha kituo hicho
kinafikia Lengo la watoto 50 kushiriki katika mbio fupi za kilometa tano zinazofahamika kama "FUN RUN"
zinazodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano Tanzania Vodacom.
Mbali na
hilo pia Panone and co. ltd imeweza kuwatengenezea watoto hao wa SALAMA
CENTRE tisheti zenye ujumbe maalumu wa
kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa watoto katika mbio hizo ujumbe ambao
unasomeka. "Let's KidsRun for fun" Pamoja na kuwapatia vifaa
mbalimbali.
Katika kuhakikisha jamii inatambua bidhaa zinazozalishwa na Panone
katika uwanja wa Ushirika kutakua na banda maalumu kwa ajili ya kuonesha
bidhaa zinazozalishwa na Panone.
No comments:
Post a Comment