Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja.
KWENU,Mastaa
wa filamu Bongo, Kajala Masanja na Wema Sepetu. Poleni kwa tifu
linaloendelea kati yenu. Hongereni kwa kazi za kila siku za kujipatia
kipato. Tuweke mambo yote pembeni, mimi kama kaka yenu, hebu tuzungumze
kirafiki kidogo leo.
Nimefuatilia kwa karibu ugomvi unaoendelea kati yenu, moyoni imeniuma na
nimeona naweza kuwashauri mawili matatu, nanyi mkiona inafaa,
muyachukue kama dira ya tatizo lililopo kati yenu.
Kwanza kabisa, kiini cha ugomvi wenyewe mpaka sasa ni kama hakina
mashiko. Ugomvi unaendeshwa kwa maneno maneno zaidi ya uhalisia.
Nilisikia eti, sababu ya ugomvi wenu ni hii; mlikutana saluni Masaki,
Kajala akiwa amelowana kwa jasho kwa vile alitokea mazoezini, Wema
alipotaka kumkumbatia, Kajala akakataa kwa nia nzuri ya kutomchafua
mwenzake – hapo bifu likaanza.
Inawezekana wakati Kajala akifanya hivyo, alikuwa na nia njema tu,
lakini Wema akahisi labda mwenzake anajisikia! Ni kawaida, hatuwezi
kufanana mioyo na mawazo.
Tatizo ni pale wanapotokea watu wengine ambao wanakuza huo ugomvi. Kuna
watu wanajiita Team Wema, hao nadhani hawana kazi. Wanakesha kwenye
mitandao ya kijamii kuchochea huo ugomvi.
Mara inasemwa sijui mmenyang’anyana bwana, mara mmepigana na mengine
mengi. Ya nini yote hayo? Kuna wakati hao Team Wema walianza kusema
Kajala anatakiwa kurudisha milioni 13 za Wema ambazo alilipa faini
mahakamani.
Jamani, thamani ya milioni 13 kwenye matatizo inafanana na kiasi kama hicho kwenye furaha? Siamini kama Wema anazitaka hizo fedha. Alizitoa kwa moyo kwa lengo la kumsaidia rafiki yake.
Jamani, thamani ya milioni 13 kwenye matatizo inafanana na kiasi kama hicho kwenye furaha? Siamini kama Wema anazitaka hizo fedha. Alizitoa kwa moyo kwa lengo la kumsaidia rafiki yake.
Niliona picha zilizopigwa mahakamani, wote mlikuwa mnamwagika machozi.
Naamini hayakuwa ya kinafiki – ilikuwa furaha. Kwa nini leo mtofautiane
kwa jambo dogo? Hata kama ni kubwa, maana inawezekana mna kitu kingine
mnachogombania ambacho sikijui, lakini bado nasema kuna kila sababu ya
kumaliza hizi tofauti.
Amini
msiamini, tofauti zenu hazina maana yoyote. Mtashindwa kufanya mambo
makubwa ya maana kwa faida yenu na kubaki mnaendekeza ugomvi ambao
mnaweza kuuepuka.
Ninyi ni binadamu, najua mna mioyo, najua kila mmoja anaamini katika
imani yake. Uadui umekatazwa kwenye vitabu vyote vitakatifu. Visasi
vimezuiwa kabisa kwenye vitabu vyote. Hekima na busara ni sifa njema.
Kusameheana ni kitu kinachoonesha uungwana wa hali ya juu kwa binadamu
mkamilifu. Bado mnayo nafasi ya kuzungumza. Hakika nawaambia, mnapoteza
mambo mengi ya maana kwa kuendekeza hilo bifu.
Hebu
tulieni, vuteni picha wakati Wema unamsaidia mwenzako pale mahakamani,
ilikuwaje? Siamini kama ulikuwa unajionyesha kuwa unazo! Sitaki kuamini
kuwa una pesa za kuchezea. Bila shaka ulikuwa ni msaada wako kwa kuguswa
na matatizo ya mwenzako.
Asitokee mtu akatumia kigezo hicho kuwagombanisha. Huu ugomvi unaweza
kuwa na faida kwa watu wengine, siyo ninyi. Mlaanini shetani.
Nawapenda sana dada zangu. Ni furaha yangu kuwaona pamoja tena mkili songesha kwenye tasnia yenu. Ni wakati wenu wa kutafakari! Inawezekana.Yuleyule,
Mkweli daima,
............................
Joseph Shaluwa
Nawapenda sana dada zangu. Ni furaha yangu kuwaona pamoja tena mkili songesha kwenye tasnia yenu. Ni wakati wenu wa kutafakari! Inawezekana.Yuleyule,
Mkweli daima,
............................
Joseph Shaluwa
No comments:
Post a Comment