KILIMANJARO serikali imetakiwa kuwashirikisha wadau wa elimu katika mabadiliko ya mfumo wa upangaji wa alama za matokeo na kuacha tabia ya kuingiza masuala ya kisiasa katika sekta ya elimu, kwani huchangia kuporoka kwa elimu nchini Tanzania.
Hayo yalibainishwa jana na mkuu wa shule ya mtakatifu Maria Goreti iliyopo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Lutrisia Njau, katika maafali ya 13 ya wanafunzi wa kidado cha nne yaliyofanyika shuleni hapo.
Njau alisema nchi inapofikia mahala na kuanza kuyumbisha usimamizi wa elimu kwa watu wake ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya mara kwa mara ya mfumo wa alama za ufaulu kwa wanafunzini bila kushirikisha wadau na kuwaandaa ni janga kubwa katika kuendeleza sekta ya elimu hapa nchini.
Aidha alisema ifike mahala wizara ya elimu na ufundi stadi nchini isimamiwe na watu wenye taaluma hiyo ambao wanauwezo wa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na sio wanasiasa kama ilivyo kwa hivi sasa.
Pamoja na suala hilo Njau alisema kumekuwa na mfumuko wa vitabu vingi vya kiada na rejea vilivyopo sokoni huku wizara ya elimu na ufundi stadi ikishindwa kutamka bayana kuwa ni vitabu vipi vinavyohitajika, jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi na waalimu.
Aidha aliitaka wizara hiyo kutoa msimo juu ya vitabu vitakavyo hitajika katika kufundishia wanafunzi wa shule za sekondari na msingi ili kuondoa mkanganyiko uliopo katika mfumo wa elimu ya Tanzania hivi sasa.
Katika hatua nyingine Njau aliitaka serikali kurejesha masuala ya elimu ya sekondari katika wizara ya elimu na ufundi stadi ili kuweza kusimamia masula yote ya elimu na kutatua changamoto zilizopo kwa hivi sasa kutokana na kwamba sekta hiyo ipo katika wizara mbili tofauti.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Shinyanga na Mwenyekiti wa kamati ya mazingira na maliasili James Lembeli, aliwataka wananchi na viongozi mbalimbali wa dini kuombea mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ili iweze kupatikana kwa amani.
Alisema katiba ya nchi ni muhimili muhimu wa kulinda taifa ambapo inatakiwa iweze kukithi mahitaji ya kizazi cha sasa na kijacho ambapo alisistiza katiba itakayo weza kikithi mahitaji hayo ni ile itakayopatikana kwa maridhiano na kushirikisha mapendekezo na maoni ya wananchi.
Alisema pasipo kuwa na maridhiano ni vikugumu kupata katiba itakayo peleka taifa mbele na kuleta maendeleo kwa wananchi na kwamba watanzania wazidi kuomba mungu ili waliopewa jukumu hilo kufanya kazi hiyo kwa busara na hekima jambo ambalo litasaidia katiba itakayo patikana itokane na maoni ya wananchi na sio vinginevyo.
No comments:
Post a Comment