Akisoma mashtaka hayo na mwendasha mashtaka mkaguzi msaidizi wa polisi Hawa Hamisi Juma, mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya Agness Mhuhando, alisema mshtakiwa faraji alimwigilia mchana, "jina tunalo" mwenye umri wa 25 kwa nguvu.
Alisema muathirika ambaye ana ulemavu wa mtindio wa ubongo, alikuwa nje ya eneo lake lakini Faraji alimshika kwa nguvu na kumwingilia ingawa binti huyo alijaribu kujinasua lakini Faraji aliendelea na unyama wake bila aibu.
Alisema ingawa mtoto wa jirani alikuwa hapo akipiga kelele mtumiwa hakutaka kumwachia alisema tukio hilo lilitokea septemba 20 mwaka huu 2014, majira ya saa 7 mchana.
Baada ya mwendesha mashtaka kumaliza maelezo yake mshtakiwa alikanusha na kesi kupigwa tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali, kesi imeahirishwa hadi 9/10/2014.
No comments:
Post a Comment